Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RSF wanapora nyumba za watu huko Khartoum - shahidi

RSF Wanapora Nyumba Za Watu Huko Khartoum   Shahidi RSF wanapora nyumba za watu huko Khartoum - shahidi

Tue, 18 Apr 2023 Chanzo: Bbc

"Wapiganaji wa RSF na makundi mengine ya watu wenye silaha wanajaribu kuingia katika nyumba ili kupora na [kuna] ripoti ambazo hazijathibitishwa za unyanyasaji wa kijinsia," anasema mwanaharakati wa haki ya kijinsia na demokrasia Hala Y Alkarib, ambaye amekuwa akikusanya ushahida kutoka kwa marafiki na wafanyakazi wenzake katika mji mkuu," Khartoum.

Aliambia kipindi cha BBC Newsday kwamba yeye na wengine wanaamini RSF haina mpangilio ya kusambaziwa chakula na mahitaji mengine kwa hivyo wanategemea uporaji.

Hakuna mtu wa kuwalinda watu, anasema, "kwa sababu jeshi la Sudan na polisi wa Sudan - wote waliokuwa washirika wa zamani wa RSF - hawana mwelekeo kabisa wa kutoa au kuendeleza ulinzi kwa raia".

Huku vibanda vikifungwa na umeme ukipotea kila mara anasema wenyeji wa Khartoum wako katika hatari kubwa - kwa sababu wengi wanategemea kwa "asilimia 100 uchumi usio rasmi" na watu wanaoishi katikati mwa jiji walilazimika kuondoka jijini ili kuweza kuweka chakula mezani lakini sasa hawawezi.

'Hakuna pa kwenda, kwa sababu ni hatari zaidi kutoka kwa sababu hakuna njia salama, hakuna maagizo kutoka kwa wanajeshi, kuhusu mahali pa kwenda.Hakuna simu za dharura.Baadhi ya watu wanajaribu kuondoka jijini lakini ni jambo gumu sana kwa sababu, kutokana na kile tunachosikia, pia kuna mapigano ambayo yanaenea karibu na Khartoum."

Hala Y Alkarib Mwanaharakati wa Haki ya Jinsia na Demokrasia.

Chanzo: Bbc