Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RRA yakusanya mapato zaidi ya lengo

53f764a5c9abe9754e6c3b0ae663884c RRA yakusanya mapato zaidi ya lengo

Tue, 10 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAMLAKA ya Mapato Rwanda (RRA) imekusanya kodi ya faranga bilioni 371.5 katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2020/2021, ikiwa ni zaidi ya lengo walilojiwekea licha ya kuwapo kwa ugonjwa wa covid-19.

Mafanikio hayo ni asilimia 105.8 ya lengo la awali walilojiwekea la faranga bilioni 351.2 sawa na faranga bilioni 20.3.

Kamishana Mkuu wa RRA, Pascal Bizimana Ruganintwali, juzi alisema mafanikio hayo yametokana na kuongezeka kwa Ushuru wa Ongezeko la Thamani (VAT) kwa kuweka mkazo kwenye teknolojia ya kukusanya kodi hususan kwa waingizaji bidhaa na viwanda.

Alisema VAT imeongezeka katika zabuni zilizotolewa na serikali katika ujenzi wa madarasa unaoendelea nchini.

Alisema ifikapo Juni mwaka huu Wizara ya Elimu ilianza ujenzi wa madarasa 22, 505 katika wilaya 30 nchini.

“Teknolojia ilisaidia mamlaka hiyo kubaini watu wanaokwepa kulipa kodi na kuchukua hatua stahili na kwa sasa wafanyabiashara wengine huduma zao zimerejeshwa,” alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz