Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RIPOTI: Takribani watu 7,500 wameuawa nchini DRC ndani ya miaka 13

Ewt.png RIPOTI: Takribani watu 7,500 wameuawa nchini DRC ndani ya miaka 13

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban watu 7,500 waliuawa kati ya mwaka 2008 na 2021, wakati wa mashambulizi 2,237 katika karibu maeneo 700, katika wilaya ya Beni, Kivu Kaskazini, na Irumu katika mkoa wa Ituri. Haya ni matokeo ya uchunguzi uliochapishwa Jumanne, Novemba 9 mjini Kinshasa kwa vyombo vya habari.

Ripoti hiyo ambayo ina kichwa cha habari “Ripoti ya Yotama kuhusu Mauaji ya Beni na Irumu, Ugaidi, Jihadi au Mauaji ya Kimbari ya Nande? ”, Utafiti huu ulifanywa na mbune wa kitaifa Tembos Yotama na mbunge wa mkoa Benze Yotama.

Katika ripoti yao ya zaidi ya kurasa 800, viongozi hao wawili waliochaguliwa katika wilaya ya Butembo wanasema wametoa wito kwa dhamiri ya kitaifa kutokana na mauaji haya ya kimbari.

Hii ni hali ngumu na ya janga, na ambapo wauaji halisi hawajatambuliwa, amesema mbunge wa kitaifa Tembos Yotama:

"Ni matukio ya kushangaza kabisa, mashambulizi yanafanywa katika maeneo yenye wanajeshi kupita kiasi, na hata serikali hadi sasa inawahusisha waasi wa ADF na mauaji hayo. Maana yake, hata serikali haina uwezo wa kutupa utambulisho wa wazi wa wauaji. "

Katika utafiti huu, wabunge hao wawili kutoka mkoa wa Kivu Kaskazini wanasema kuwa kabila moja limelengwa kwa 95%.

"Ikiwa watu kutoka jamii ya Nande wanalengwa, ni kwa sababu wamepinga kwa muda mrefu utumiaji wa nchi yetu wa vitendo vya ukatili," wamesema.

Wamependekeza kwamba serikali iandae mikakati mipya ya kukomesha ukatili huu. Ili kukomesha ukatili huu, wabunge hawa wawili wanapendekeza kwa serikali "kupitia upya, kurekebisha mkakati huu, kwa sababu mauaji ya watu wengi yameongezeka kwa kiasi kwamba tunaelekea kuamini kuwa hatua hii haifai kwa usalama wa mashariki. "

Wanapendekeza kwa jumuiya ya kimataifa kuundwa kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa ajili ya DRC na "kuanzishwa kwa uchunguzi huru wa kimataifa, ili kubaini wauaji halisi, ili wafikishwe mahakamani, na kwamba haki itendeke katika hali sawa. "

Utafiti huu ulifanyika kwa ushirikiano na taasisi ya Wakili Mbenze Yotama na kituo cha kukuza demokrasia, sheria na maendeleo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live