Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RIPOTI: Simu za maafisa wa magereza zilizimwa wakati magaidi wakitoroka

3bc747e2414f31d8 RIPOTI: Simu za maafisa wa magereza zilizimwa wakati magaidi wakitoroka

Tue, 30 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutoroka kwa washukiwa watatu wa ugaidi kutoka gereza kuu la Kamiti mnamo Novemba 14, kumelipaka tope jeshi hilo baada ya ripoti mpya kuonesha kuwa simu za maboss wa gereza hilo zilizimwa au kutopatikana wakati tukio hilo linatokea.

Kamishna wa idara ya magereza nchini Wycliffe Ogalo na mkuu wa gereza la Kamiti Charles Mutembei hawapukatikana kwa simu baada ya washukiwa wa ugaidi kutorokaTukio hilo lilisalia kuwa siri kubwa Waziri Fred Mating’i akijulishwa baadaye, yeye na Rais Uhuru Kenyatta wakighadhabishwa na Ogalo na kumtimua Mutembei.

Mkuu wa gereza la Kamiti Charles Mutembei hakupatikana kwa simu, na kwa wasiwasi, maafisa katika gereza hilo wakajaribu kumtafuta kamishna wa idara ya magereza nchini Wycliffe Ogalo, naye vilevile hakupatikana.

Kwa mujibu wa nakala ya Jumapili ya gazeti la Nation, maafisa wa gereza hilo walilazimika kuwatumia wakubwa wao jumbe kutumia mtandao wa WhatsApp wakiendelea na uchunguzi kubaini ni vipi washukiwa hao walifanikiwa kutoroka.

Ukosefu wa mwongozo kutoka kwa wakubwa wao kunadaiwa kulemaza uchunguzi wa maafisa hao kwani wote walikuwa katika hali ya wasiwasi.

Tukio hilo lilisalia kuwa siri kubwa hadi Jumatatu ya Novemba 15, saa kumi alasiri, Ogalo alipompigia simu Waziri wa Usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’i kumjulisha kuhusu kutoroka kwa watatu hao.

Ukosefu wa mbinu mwafaka ya kushughulikia suala hilo, kuchelewa kufika Kamiti kuongoza oparesheni ya kuwasaka watoro, na ukosefu wa yeyote aliyeelewa kilichojiri hadi watatu hao kutoroka hakukuwapendeza Matiang’i na Rais Uhuru Kenyatta.

Matiang’i alimpigia simu Rais Kenyatta chini ya dakika tano, na kuita mkutano na kamati ya kitaifa ya usalama kujadili suala hilo.

Baada ya mkutano na kuufahamisha umma kuhusu tukio hilo, Matiang’i, katibu wa magereza Zeinab Hussein na mwenzake wa usalama Karanja Kibicho walielekea Kamiti ambako Ogalo na Mutembei walitatizika kuelezea ni lini walijulishwa kuhusu kutowekwa kwa watatu hao.

Matiang’i alimuarifu Rais Kenyatta kuhusu kilichojiri na ikaamuliwa kuwa Ogalo angetimuliwa kazini.

Awali, iliripotiwa kuwa idara ya DCI ilitangaza zawadi ya shilingi milioni 60 kwa yeyote aliyekuwa na taarifa ambayo ingefanikisha kukamatwa kwa watatu hao.

“Utoro gerezani! Zawadi ya shilingi milioni 60 itatolewa kwa yeyote aliye na taarifa itakayowezesha kukamatwa kwa washukiwa watatu wa ugaidi waliotoroka kutoka gereza kuu la kamiti saa saba usiku,” idara ya DCI ilisema kwenye mtandao wa Twitter.

Mmoja wa washukiwa hao ni Musharaf Abdalla Akhulunga almarufu Shukri kutoka Mumias, Kaunti ya kakamega na ambaye alikamatwa mwaka 2012 akilenga kutekeleza shambulizi kwenye makao ya bunge.

Mwingine ni Mohamed Ali Abikar aliyekamatwa kwa kuhusika katika shambulizi katika chuo kikuu cha Garissa Aprili 2015.

Wa tatu ni Joseph Juma Adhiambo almaarufu Yusuf aliyenaswa mwaka akienda kujiunga na Al Shabaab.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live