Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RAIS RAMAPHOSA AMTEUA MO DEWJI KUWA MSHAURI WAKE

Moo?fit=800%2C445 RAIS RAMAPHOSA AMTEUA MO DEWJI KUWA MSHAURI WAKE

Thu, 8 Apr 2021 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amemteua mfanyabiashara kijana nchini, Mohamed Dewji (Mo) kuwa kwenye jopo lake la watu watano kumshauri kuhusu masuala ya uchumi na uwekezaji.

Dewji, ambaye hivi karibuni Jarida maarufu la Forbes limemtaja kuwa bilionea kijana wa 13 kati ya 18 barani Afrika, ameingia kwenye jopo hilo ambalo lengo ni kupanga mikakati ya namna bora ya kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya Afrika Kusini.

Taarifa kwa vyombo vya habari jana, imeeleza kuwa Mo Dewji, anayemiliki kampuni ya Mohamed Enterprises Limited (MeTL), atakuwa kwenye chombo hicho kwa kipindi cha miaka mitano.

Imesema kuwa uamuzi wa Ramaphosa kumteua Mo Dewji kuwa mshauri wake umetokana na kuvutiwa na jitihada za mfanyabiashara huyo maarufu nchini, kubobea kwenye masuala ya uchumi, huku akiifanya MeTL kuwa miongoni mwa kampuni bora Afrika.

Pia, uteuzi huo umeelezwa kuwa unatokana na Ramaphosa kuthamini na kutambua mchango wa Mo katika uwekezaji ambao umekuwa kichocheo kwa uchumi wa mataifa mbalimbali Afrika.

“Ninayo furaha kubwa kukujulisha kwamba, nimekuteua kwenye Baraza la Ushauri la Rais kuhusu uwekezaji ambalo lina jukumu kubwa kuhakikisha Afrika Kusini inapiga hatua kiuchumi na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Chanzo: zanzibar24.co.tz