Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Putin aunga mkono ujumbe wa amani wa Afrika - Ramaphosa

Putin Aunga Mkono Ujumbe Wa Amani Wa Afrika   Ramaphosa Putin aunga mkono ujumbe wa amani wa Afrika - Ramaphosa

Thu, 8 Jun 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wamezungumza kwa njia ya simu kuhusiana na ujumbe ujao wa amani wa viongozi sita wa Afrika nchini Urusi na Ukraine.

"Rais Putin aunga mkono ujumbe wa amani wa Afrika - Ramaphosa mpango wa wakuu wa nchi za Afrika na kueleza nia yake ya kupokea ujumbe wa amani,” taarifa kutoka ofisi ya rais wa Afrika Kusini ilisema.

Mpango wa wakuu wa nchi za Afrika na kueleza nia yake ya kupokea ujumbe wa amani,” taarifa kutoka ofisi ya rais wa Afrika Kusini ilisema.

Siku ya Jumanne, viongozi wa Afrika waliohusika walikuwa na majadiliano "kutafuta njia za kumaliza mzozo", iliongeza.

Viongozi wengine walioungana na jitihada za kuleta amani wanatoka Comoro, Misri, Senegal, Uganda na Senegal - na kulingana na taarifa kutoka kwa rais siku ya Jumatano, wote walisema wanaweza kusafiri katikati ya Juni.

"Viongozi walikubaliana kwamba watashirikiana na Rais Putin na Rais [Volodymyr] Zelensky juu ya vipengele vya kusitisha mapigano na amani ya kudumu katika eneo hilo."

Mawaziri wao wa mambo ya nje sasa walikuwa katika harakati za kukamilisha vipengele vya ramani ya mpangokazi wa kuelekea amani, iliongeza.

Mkutano wa kilele wa Urusi na Afrika umepangwa kufanyika mwishoni mwa Julai huko St Petersburg, ofisi ya rais ilisema.

Chanzo: Bbc