Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa wa chuo anayechomelea vyuma

Profesa Vyuma Chuma.png Profesa wa chuo anayechomelea vyuma

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Profesa Kabir Abu Bilal, wa chuo kikuu kimoja nchini Nigeria, ameamua kujiajiri kwa kuchomelea vyuma licha ya kuwa ni mtumishi wa taasisi hiyo ya elimu iliyopo Kaskazini mwa Jiji la Zaria nchini humo.

Profesa Bilal ameieleza BBC Swahili kwamba haoni aibu kufanya kazi ya uchomeleaji licha ya kuwa ni profesa.

"Ninapata pesa zaidi kutokana na uchomaji vyuma," amesema Profesa Bilal.

Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 50 anafundisha na kusimamia wanafunzi wa utafiti katika kitivo cha uhandisi katika Chuo Kikuu cha Ahmadu Bello, ambacho ni chuo kikuu kikubwa zaidi nchini Nigeria.

Amefanya kazi chuo kikuu kwa miaka 18 sasa na kuchapisha vitabu kadhaa vya fizikia na uhandisi wa umeme.

Msomi mwenzake, Profesa Yusuf Jubril, ameeleza kuwa jamii inafikiri mtu akiwa na kiwango kama hicho cha elimu kuna majukumu fulani siyo yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live