Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Afrika Kusini achaguliwa kuwa jaji Umoja wa Mataifa

Profesa Afrika Kusini Achaguliwa Kuwa Jaji Umoja Wa Mataifa Profesa Afrika Kusini achaguliwa kuwa jaji Umoja wa Mataifa

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Profesa wa sheria wa Chuo Kikuu cha Pretoria Dire Tladi ameweka historia kwa kuwa Mwafrika Kusini wa kwanza kuchaguliwa kuwa jaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ya Umoja wa Mataifa.

Rais Cyril Ramaphosa mnamo Ijumaa alisifu uchaguzi wa Prof Tladi kama "mafanikio bora ya kibinafsi ambayo taifa linashiriki kwa fahari kubwa".

Yeye ni mmoja wa majaji watano waliochaguliwa siku ya Alhamisi na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama kwa mihula ya miaka tisa, kuanzia Februari mwaka ujao.

ICJ ndiyo chombo kikuu cha mahakama cha Umoja wa Mataifa, kinachotoa ushauri wa kisheria kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa na kutatua mizozo ya kisheria kati ya nchi.

Ili kuchaguliwa, wagombea lazima wapate wingi kamili katika Mkutano Mkuu na Baraza la Usalama.

Wagombea wengine watatu wa Kiafrika kutoka Zambia, Misri na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hawakuchaguliwa kuwania nafasi hiyo.

Chanzo: Bbc