Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prince Charles awasili Rwanda kuhudhuiria mkutano Jumuiya ya Madola

Prince Rwanda Madola Prince Charles awasili Rwanda kuhudhuiria mkutano Jumuiya ya Madola

Wed, 22 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamfalme wa Wales na Duchess wa Cornwall wamewasili Rwanda kabla ya mkutano wa kilele wa viongozi wa Jumuiya ya Madola.

Prince Charles anamuwakilisha Malkia, mkuu wa Jumuiya ya Madola, katika hafla hiyo, ambayo iliahirishwa mwaka 2021 na 2020 kwa sababu ya janga la corona.

Safari hiyo inaashiria ziara ya kwanza ya kifalme nchini Rwanda, ambayo ni moja ya mataifa machache ambayo Malkia hajatembelea.

Haya yanajiri baada ya kuripotiwa kuwa mwanamfalme huyo alikosoa kwa siri mpango wa Uingereza wa kutuma waomba hifadhi nchini Rwanda.

Kulingana na madai yaliyoripotiwa na gazeti la Times mapema mwezi huu, mrithi wa kiti cha ufalme alisemekana kuamini kuwa sera hiyo ilikuwa "ya kutisha".

Safari ya kwanza ya ndege iliyopaswa kuchukua waomba hifadhi kutoka Uingereza hadi Rwanda ilisitishwa wiki iliyopita, dakika chache kabla ya ndege kupaa, kufuatia maamuzi ya kisheria ya mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya.

Prince Charles na Camilla waliwasili katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali, Jumanne usiku na kulakiwa na kikundi kidogo cha watu mashuhuri.

Katika ziara hiyo, mrithi wa kiti cha ufalme atakutana na manusura na wahusika wa mauaji ya kimbari ya Rwanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live