Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yawasaka Gen Z waliochoma Bunge

Gen Z  AWS Gen Z

Thu, 4 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idara ya Uchunguzi wa Jinai nchini Kenya imechapisha picha za vijana 38 wanaotafutwa kwa kufanya uharibifu wakati wa maandamano ya kupinga mswada wa fedha nchini humo.

Mamlaka hiyo ilisema katika chapisho lake kwenye mitandao ya kijamii kuwa, "Watu ambao picha zao zinaonekana hapa chini wanatafutwa na polisi kwa shughuli zao haramu wakati wa maandamano ya kupinga muswada wa fedha mwaka 2024."

Waliomba kila mmoja wao kuripoti kituo cha polisi kilicho karibu kwa hatua zaidi za kisheria.

Kenya ilirejea tena katika vichwa vya habari Duniani baada ya maandamano mabaya kutokea kwa siku za hivi karibuni yakioongozwa na kizazi cha Gen Z kupinga muswada wa fedha. Waandamanaji hao wameendelea na matukio ya kushtukiza kwa wiki ya tatu mfululizo.

Ghasia zimeonekana kuongezeka licha ya Rais William Ruto kuondoa mapendekezo ya kodi Juni 26. Mapendekezo hayo yalitajwa kuwa msingi wa maandamano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: