Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yatawanya maandamano ya Wanaharakati

Image 150 1140x640.png Polisi yatawanya maandamano ya Wanaharakati

Thu, 19 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetumia nguvu kutawanya maandamano yaliyofanyika katika mji wa Goma uliopo mashariki mwa nchi hiyo, yaliyokuwa yakipinga uwepo wa vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika eneo hilo.

Katika maandamano hayo, Watu wapatao 100 walikusanyika karibu na makutano ya barabara kwa ajili ya kuandamana dhidi ya vikosi hivyo, wanavyovishutumu kushindwa kufanya kazi na kudorola kwa amani ya eneo hilo.

Miezi ya hivi karibuni, maelefu ya wanajeshi wa Kenya na Burundi walipelekwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kulisaidia jeshi la nchi hiyo na walinda amani wa Umoja wa Mataifa, kupambana na makundi ya waasi katika eneo lenye machafuko.

Hata hivyo, mmoja wa waandamanaji Josue Waalay kutoka kundi la Vijana wanaharakati amesema, wanajeshi wa Afrika Mashariki hawafanyi chochote zaidi ya kuwalinda watu aliowaita maadui.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live