Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yamdaka anayedaiwa kuua baba, mama, watoto watatu

Polisi Watatu Polisi yamdaka anayedaiwa kuua baba, mama, watoto watatu

Tue, 27 Jun 2023 Chanzo: Mwananchi

Polisi wamemkamata mshukiwa aliyehusika na mauaji ya wanafamilia watano wiki iliyopita katika Wilaya ya Masaka nchini Uganda.

Polisi wanasema mtuhumiwa huyo, ambaye ni mpwa wa mganga wa kienyeji, Emmanuel Ssalongo anayeishi Kitongoji cha Buwunga huko Masaka, alikuwa akilipiza kisasi kufuatia kifo cha mama yake.

"Taarifa tulizopata zinaonyesha kuwa hili linaweza kuwa ni shambulio la kulipiza kisasi. Mtuhumiwa alimshambulia mjomba wake (Ssalongo) ili kulipiza kisasi cha kifo cha mama yake ambaye anadai mjomba alimroga na kumuua miaka miwili nyuma," Msemaji wa Polisi, Fred Enanga amewambia waandishi wa habari jijini Kampala jana.

Mnamo wiki iliyopita wanafamilia watano waliuawa kwa kukatwa mapanga huko Masaka, Uganda.

"Mtuhumiwa alikamatwa na vikosi vyetu akiwa mafichoni, Jeshi la Polisi linaendelea kumhoji zaidi ili kubaini kama kulikuwa na watu wengine waliohusika na mauaji haya," alisema.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwaua Ssalongo, 57, na wanafamilia wengine wanne. Polisi waliwataja waliofariki kuwa ni mke wa Ssalongo, Proscovia Ndagaano, (52) Beatrice Nakalyango (13) na wajukuu wawili Shivan Nakasagga, (5) na Robert Kayemba (2).

Enanga alisema Nakalyango na Nakasagga walibakwa na kisha kukatwakatwa hadi kufa.

Ssalongo na familia yake walishambuliwa Jumamosi asubuhi na kukatwakatwa hadi kufa.

Chanzo: Mwananchi