Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wengine watano wakamatwa kwa tuhuma za mauaji ya wageni wa Ruto

Ruto Ateua Rais Ruto

Sun, 30 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maofisa wengine watano wa polisi wamekamatwa kuhusiana na mauaji ya kinyama ya wageni wawili wa Rais William Ruto waliofika nchini Julai 2022 kusaidia katika masuala ya ICT ya kampeni zake.

Mahakama ya Kahawa inayoamua kesi za ugaidi ilifahamishwa Alhamisi kwamba maafisa hao watano wa polisi walikuwa miongoni mwa makachero waliokuwa wanawaandama na kuchunguza mienendo ya Mohammed Said Sami na Zulfiqar Ahmed kutoka India waliouawa pamoja na dereva wa teksi Nicodemus Mwania aliyekuwa akiwabeba.

Mahakama ilielezwa maafisa hao wa kitengo maalum cha uchunguzi- SSU- katika Idara ya Kuchunguza Uhalifu (DCI) kilichovunjwa Mabw  John Mwendwa Mbaya, David Chepcheng Kipsoi, Stephen Luseno Matunda, Paul Njogu Muriithi na Simon Gikonyo walihusika katika mauaji na utupaji wa maiti za watatu hao katika msitu wa milima ya Abadares.

Upande wa mashtaka uliomba washukiwa hao wazuiliwe kwa siku 30 kuwezesha uchunguzi kukamilishwa.

Ombi la kuwazuia washukiwa hao kwa siku 30 lilipingwa na wakili Danstan Omari huku akiomba muda kujibu ombi la kitengo cha masuala ya usimamizi katika idara ya polisi (IAU) wahojiwe kwa siku 30.

Hakimu mkuu mahakama ya Kahawa atatoa uamuzi Oktoba 31, 2022 (Jumatatu) ikiwa ataruhusu ombi hilo la IAU.

Kukamatwa kwa watano hao John Mwendwa Mbaya, David Chepcheng Kipsoi, Stephen Luseno Matunda, Paul Njogu Muriithi, na Simon Gikonyo waliokuwa katika kitengo cha SSU kumefikisha tisa polisi wanaozuiliwa kuhusiana na mauaji ya wageni hao wa Rais Ruto.

Wahasiriwa hao Mohammed Said Sami na Zulfiqar Ahmed kutoka India ambao walikuwa wataalam wa masuala ya mawasiliano ICT walitekwa nyara pamoja na dereva teksi Nicodemus Mwania nje ya hoteli moja Nairobi na hatimaye wakapigwa risasi na kuuliwa katika msitu wa Aberdare.

Ijumaa wiki hii hakimu mkuu Bi Diana Mochache alikubalia ombi la IAU kuendelea kuwachunguza maafisa wengine wane waliokamatwa kuhusiana na mauaji hayo ya Sami na Ahmed.

Mochache alisema idara hiyo ya IAU iko na uwezo wa kutoa maamuzi iwapo washukiwa hao wane wanapasa kushtakiwa au la baada ya kukamilisha uchunguzi.

Bw Omari alikuwa amepinga IAU kikiendelea na uchunguzi huo kwa vile masuala ya utovu wa nidhamu wa maafisa wa polisi uchunguzwa na mamlaka huru ya polisi IPOA ama afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma DPP.

Baada ya hakimu kuruhusu IAU iendelee kuchunguza washukiwa hao, Bw Omari alikata  rufaa katika mahakama kuu ya kiambu akidai haki za maafisa hao wa polisi zinakandamizwa.

Uamuzi wa mahakama kuu kutolewa Jumatatu.

Afisa anayechunguza kesi ya maafisa hao watano Bw Wilhem Kibet, alidai katika afidaviti iliyowasilishwa kortini kwamba washukiwa hao walitajwa kuhusika na mauaji ya raia hao wawili kutoka India na dereva wa teksi marehemu Mwania.

Bw kibet anadai kachero Mbaya alikuwa na Bw Kipsoi aliyeamriwa asalie katika hoteli ya  Ole Sereni Hotel kuchunguza mienendo ya Sami na Ahmed.

Amedokeza Mabw Matunda, Murithii, na Gikonyo walishiriki katika mauaji hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live