Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wavamia ofisi za DP Ruto

Ruto Urais Polisi wavamia ofisi za DP Ruto

Mon, 25 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi wa Kenya katika mji mkuu Nairobi wamevamia ofisi zinazoaminika kuwa na uhusiano na naibu wa rais wa nchi hiyo, William Ruto, ambaye ni mmoja wa wagombea wakuu katika uchaguzi wa mwezi ujao.

Afisa wa polisi alisema wapelelezi wamekamata kompyuta mbili na seva mbili.

Afisa katika sekretarieti ya kampeni ya naibu rais aliiambia BBC kwamba hawatataka kuvutiwa na kile alichokitaja kuwa ‘’maonyesho tu kwa umma na usumbufu’’.

Uvamizi huo unajiri huku kukiwa na mvutano kati ya vikosi vya usalama nchini na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini (IEBC).

Mwishoni mwa juma mkuu wa tume hiyo alikosoa vikali uamuzi wa kuwazuilia raia watatu wa kigeni ambao walikuwa wamepewa kandarasi ya kufanyia kazi mfumo wa kielektroniki wa kupiga kura nchini.

Polisi hao walipuuzilia mbali madai ya IEBC, wakisema hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa tume hiyo ya uchaguzi ilikuwa na kandarasi ya watatu hao au kwamba walikuwa wafanyikazi wa kampuni iliyopewa kandarasi na tume hiyo.

Kinyanganyiro cha urais kinaonekana kuwa mchuano mkali kati ya Bw Ruto na aliyekuwa waziri mkuu, Raila Odinga

Chanzo: www.tanzaniaweb.live