Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi watumia mabomu kutawanya waandamanaji 'mfumuko wa bei'

Polisi Mabomu Uganda (600 X 277) Raia waaandamana kupinga mfumuko wa bei, Polisi wawatawanya kwa mabomu

Tue, 26 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi nchini Uganda wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya raia walioandamana katika Miji Mitatu kupinga kupanda kwa bei ya mafuta na vyakula muhimu huku wakiwashikilia watu kadhaa.

Maandamano hayo ni ya pili katika mwezi mmoja ambapo waandamanaji wamejitokeza barabarani katika Miji ya Jinja, Kamuli na Luuka kuonesha hasira zao juu ya kupanda kwa gharama ya maisha nchini humo.

Hata hivyo Rais Yoweri Museveni amesema kupunguzwa kwa kodi au kutoa ruzuku ili kujaribu kudhibiti mfumuko wa bei kungefanya hali kuwa mbaya zaidi kwa kuwapa watu "faraja ya bandia"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live