Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi watatu wa Kenya kuhukumiwa kwa mauaji ya wakili

Polisi Watatu Wa Kenya Kuhukumiwa Kwa Mauaji Ya Wakili Polisi watatu wa Kenya kuhukumiwa kwa mauaji ya wakili

Fri, 3 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Mahakama nchini Kenya inatarajiwa kutoa hukumu kwa polisi wa zamani watatu wa kenya na raia mmoja kuhusiana na mauaji ya wakili maarufu wa masuala ya haki za binadamu Willie Kimani na raia.

Wanne hao,Fredrick Leliman, Stephen Cheburet, Sylvia Wanjiku na Peter Ngugi, walipatikana na hatia ya mauaji ya Bw kimani, mteja wake Josephat Mwendwa na dereva wa teksi Joseph Muiruri.

Mke wa marehemu wakilina familia yake tayari wamewasili kwenye mahakama katika mji mkuu, Nairobi.

Miili ya Bw Kimani na watu wengine wawili ilipatikana baaya ya kutupwa mtoni viungani mwa mji mkuu , Nairobi.

Wakili Kimani alikuwa akimteteaMwendwa, ambaye ni dereva wa pikipiki ambaye alikuwa anamshutumu Bw Leliman - mmoja wa maafisa watatu wa polisi waliopatikana na hatia – kwa kumpiga risasi bila sababu katika kituo cha ukaguzi wa magari mnamo mwaka 2015.

Bw Kimani , Bw Mwendwa na Bw Muiruri walionekana kwa mara ya mwisho tarehe 23 Juni 26 kwenye kituo cha polisi.

Miili yao iliyokatwa iligundulika wiki mbili baadaye katika mto uliopo takriban kilomita 100(maili 62) kutoka mji mkuu.

Hukumu hii inakuja wakati huduma ya polisi nchini Kenya ikichunguzwa zaidi kuhusiana na mauaji ya kiholela na utekaji nyara.

Rais William Ruto tayari amevunja vikosi kadhaa maalum vya polisi vinavyoshutumiwa kwa mauaji na utekeji wa raia.

Chanzo: Bbc