Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi watanda maeneo mbalimbali Kenya hofu ya maandamano

Polisi Watanda Maeneo Mbalimbali Kenya Hofu Ya Maandamano Polisi watanda maeneo mbalimbali Kenya hofu ya maandamano

Fri, 7 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Polisi wengi wameonekana kuzunguka katika maeneo ya mji mkuu wa Kenya, Nairobi, na miji mingine mikuu huku wafuasi wa upinzani wakitarajiwa kufanya maandamano kupinga gharama kubwa za maisha.

Maandamano yameripotiwa katika maeneo kadhaa ikiwemo Nairobi, Mombasa na Kisumu, ambapo polisi wametumia vitoa machozi kuwatawanya watu wengi.

Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa biashara kadhaa zimeharibiwa na waandamanaji mjini Kisumu.

Makabiliano kati ya polisi na waandamanaji yameripotiwa katika maeneo kadhaa ya Nairobi, na barabara kuu yenye shughuli nyingi kuelekea mjini ilikuwa imefungwa asubuhi.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga anatarajiwa kuhutubia katika mkutano mkuu wa kisiasa katika mji mkuu baadaye.

Anatarajiwa kutangaza kuanza tena kwa maandamano ya kila wiki ya nchi nzima.

Mamlaka imeruhusu mkutano huo kuendelea lakini ikaonya dhidi ya waandamanaji wanaoingia katikati mwa jiji la Nairobi.

Bw Odinga anatarajiwa kuanzisha kampeni ya kukusanya saini kuunga mkono juhudi zake za kulazimisha serikali kupunguza bei ya bidhaa muhimu kama vile petroli.

Maandamano hayo yanakuja baada ya Rais William Ruto kutia saini nyongeza ya ushuru yenye utata - ikiwa ni pamoja na ile ya mafuta - kuwa sheria.

Chanzo: Bbc