Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wapata mwili wa binti aliyeuawa, baada ya gari kukwama matopeni

Ba8d78f96a95b2d9 Polisi wapata mwili wa binti aliyeuawa, baada ya gari kukwama matopeni

Sat, 17 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Nyokabi aliondoka nyumbani kuenda kukutana na mpenziwe lakini hakurudi na baadaye mwili wake ukapatikana kwenye gari

- Polisi wanaamini mpenziwe alikuwa akielekea kichakani kuutupa mwili huo wakati gari lake liliingia matopeni

- Binti huyo amemwacha mtoto msichana wa miaka sita na familia yake inaomba haki kutendeka kwao

Makachero wa DCI wamemtia mbaroni jamaa mwenye miaka 38 kuhusiana na kifo cha mpenziwe wa miaka 25.

Kulingana na ripoti ya DCI, Evans Karani anazuiliwa kuhusiana na kifo cha aliyekuwa mpenziwe Catherine Nyokabi.

Mwili wa Nyokabi ulipatikana kwenye gari lake katika barabra moja eneo la Juja ukiwa na umekatakatwa na kuchomwa.

Polisi wanashuku Karani alikuwa kwenye safari ya kuenda kuutupa mwili huo kichakani wakati gari lake lilikwama kwenye matope.

Mvua ilikuwa imenyesha na kufanya barabara ya Bob Harris Juja kuwa mbaya na hivyo gari hilo likaingia matopeni.

Tayari Karani anaripotiwa kukiri kwa maafisa wa polisi kuwa alitekeleza mauaji hayo baada ya tofauti za kimapenzi.

Bababke Nyokabi aliambia gazeti la Standard kuwa alimjua Karani kama mpenzi wa mwanawe na walikuwa na mzozo wa kimapenzi.



"Niliwajua kama wapenzi. Na kama vile mahusiano mengine ya kimapenzi walikuwa na mizozo hapa na pale. Wiki mbili zilizopita, msichana wangu alianiambia walikuwa wametofautiana.

"Aliniambia walikuwa wameachana na nikwambia ni sawa kwani hakuna haja ya kuwa kwenye uhusiano ambapo kuna masaibu," alisema mzee huyo.

Mshukiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji Jumatatu Aprili 19.

Kulingana na taarifa kutoka kwa majirani, Nyokabi aliondoka nyumbani na ksuema ameenda kukutana na mpenziwe.

Nyokabi amemwacha mtoto wa kike wa miaka sita huku familia yake ikiomba haki itendeke katika suala hilo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke