Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wapambana na waandamanaji Senegal

Senegal Polisiiiiiii Polisi wapambana na waandamanaji Senegal

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafuasi wa vyama vya upinzani na polisi wamepambana katika mji mkuu wa Senegal Dakar baada ya Rais Macky Sall kutangaza kuakhirisha kwa muda usiojulikana uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Februari 25, na hivyo kuzusha wasiwasi kimataifa. Siku ya Jumapili, kwa kuitikia wito wa baadhi ya wagombea wa upinzani, mamia ya wanaume na wanawake wa marika yote, wakipeperusha bendera za Senegal au kuvaa jezi ya timu ya taifa ya soka ya nchi hiyo walikusanyika mapema alasiri kwenye mzunguko wa barabara kwenye mojawapo ya barabara kuu za mji mkuu Dakar.

Polisi walikabiliana na waandamanaji kwa kufyatua mabomu ya kutoa machozi na kisha kuwafukuza waandamanaji waliokuwa wakikimbia kupitia barabara zinazopakana, huku baadhi ya waandamanaji wakijibu mapigo kwa kurusha mawe.

Mbali na hayo, vikosi vya usalama vya Senegal vimemkamata mgombea urais Anta Babacar Ngom karibu na eneo la maandamano. Hayo yameelezwa na meneja wake wa kampeni.

Siku moja tu kabla ya kuanza kwa kampeni rasmi, Rais Sall alilitumbukiza taifa kwenye hatima isiyojulikana, alipotangaza kuwa ameamua kuingilia kati kwa sababu ya mzozo uliopo kati ya Bunge na Mahakama ya Katiba kuhusu kukataliwa kwa baadhi ya wagombea.

Wabunge wanawachunguza majaji wawili wa Mahakama ya Katiba ambao uadilifu wao katika mchakato wa uchaguzi umetiliwa shaka. Rais Macky Sall

"Nitaanzisha mazungumzo ya wazi ya kitaifa ili kuleta pamoja masharti ya uchaguzi huru, wa wazi na shirikishi," alieleza Rais Sall siku ya Jumamosi bila kutaja tarehe mpya ya uchaguzi huo.

Wagombea urais wamesema watazindua kampeni zao siku ya Jumapili kukhalifu agizo rasmi la kuahirishwa uchaguzi.

Chama cha upinzani cha RFM kimesema kinapinga "kiutaratibu" kuakhirishwa kwa uchaguzi wa rais.

"Tutaonana na watu wote wa Senegal Jumapili hii kwa maandamano," ameeleza msemaji wa chama hicho Cheikh Tidiane Youm.

Habib Sy, mmoja wa wagombea 20 amesema vyama vya upinzani vimekutana na kukubaliana kuzindua kampeni zao za uchaguzi pamoja.

Mpinzani mwingine, meya wa zamani wa Dakar Khalifa Sall, yeye ametoa wito kwa nguvu za kidemokrasia kuungana.

"Senegal yote lazima isimame pamoja," amesema Sall mbele ya waandishi wa habari.

Sall, ambaye hana uhusiano wa nasaba na rais wa nchi hiyo, ameshutumu kile alichokiita "mapinduzi ya kikatiba" ya kiongozi ambaye "ana ndoto za kubaki milele".

Marekani, Umoja wa Ulaya na Ufaransa zimetoa miito ya kutaka tarehe mpya ya uchaguzi iwe ya mapema zaidi kadiri iwezekanavyo.

Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imeeleza kutiwa "wasiwasi' na uamuzi huo wa Rais Sall na kutoa wito wa kufanyika mazungumzo.../

Chanzo: www.tanzaniaweb.live