Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wanaonya wafuasi wa Bobi wine sherehe yake ya kumkaribisha

Polisi Wanaonya Wafuasi Wa Bobi Wine Sherehe Yake Ya Kumkaribisha Polisi wanaonya wafuasi wa Bobi wine sherehe yake ya kumkaribisha

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Polisi katika mji mkuu wa Kampala Uganda wamewaonya wafuasi wa mwanasiasa wa upinzani nchini humo na mwanamuziki Bobi Wine, kufuata sheria wanapomkaribisha mwanasiasa huyo

Hii ni baada ya viongozi wa chama cha Bobi Wine, NUP wakiongozwa na sehemu ya wabunge wa chama hususan wale wanaowakilisha maeneo ya bunge la Kampala mjinikuwahamasisha watu kujitokeza kwa wingi kote nchini na kukusanyika katika wanja wa ndege wawa kimataifa wa Entebbe na barabara za Entebbena barabara nyingine zinazoelekea kwenyemakazi ya Bobi Wineya Wakiso kumpokea.

Bw David Sserukenya, mbunge wa Makindye Ssabagabo, alibainisha kuwa wafuasi wa Bw Kyagulanyi wameamua kuandaa sherehe kubwa ya kumkaribisha kama njia ya kumpongeza kwa ziara zake za uhamasishaji ambazo amezifanya nchini Uganda na nje ya nchi kwa muda wa mwezi mmoja uliopita.

‘’Ninaomba wafuasi wa Bw Kyagulanyi waheshimu sheria za barabarani na miongozo ya usalama , wakati wa hafla hii. Hili litakua jaribio kwa vyombo vyetu vya usalama, lakini tunatarajia wataheshimu sheria na kuimarisha utulivu huku Waganda wakitekeleza haki zao siku huu,’’alisema .

Lakini Naibu Msemaji wa polis iwa jiji la Kampala , Bw Luke Owoyesigyire alinukuliwa na gazeti la Daily Monitor nchini humo akisema’’ Sijui hili [karamu ya kumkaribisha Bobi Wine], lakini maandamano yoyote yasiyo halali yatashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.’’

Polisi wanatarajia pia kutoa taarifa rasmi kuhusu suala hilo Jumatano, kulingana na Bw Owoyesigyire.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa X (zamani ikiitwa Twitter ), Bw Kyagulanyi alithibitisha Jumanne kuwa atawasili ‘’Oktoba 5, 10.00AM’’

Chanzo: Bbc