Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wamsaka Mukhisa Kituyi kufuatia tuhuma ya kumpiga mpango wake wa kando

7181dfe780b7dba1 Polisi wamsaka Mukhisa Kituyi kufuatia tuhuma ya kumpiga mpango wake wa kando

Tue, 15 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mukhisa Kituyi alikosa kufika katika afisi za DCI, Nyali kuandikisha taarifa kuhusu tuhuma dhidi yake ya kupiga na kujeruhiDiana Opemi Lutta kupitia ripoti aliyowasilisha katika Kituo cha Polisi cha Nyali alidai kuwa Mukhisa Kituyi alimpiga mangumi na mateke baada ya kukataa kushiriki ngono naye Mnamo Alhamisi, Juni 10, Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai alimuita Kituyi kufuatia madai hayo

Makachero wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kutoka Nyali, Mombasa, wameanza kumsaka mgombeaji wa urais 2022 Mukhisa Kituyi kuhusiana na kesi dhidi yake ya kupiga na kujeruhi.

Hii ni baada ya Kituyi kukosa kufika katika afisi za DCI, Nyali kuandikisha taarifa kuhusu tuhuma dhidi yake ya kupiga na kujeruhi.

Mkuu wa Polisi eneo la Pwani Paul Ndambuki aliambia gazeti la People Daily kuwa maafisa wake wanasmaka Katibu huyo wa zamani wa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Maendeleo (UNCTAD) kukosa kufika mbele yao kama alivyoarifiwa Alhamisi, Juni 10.

“Kituyi anaoneka kuwa mkaidi na hatua nyingine itakayochukuliwa ni kuwatuma makachero kutoka kwa kituo ambacho mlalamishi aliwasilisha ripoti wakishirikiana na maafisa wa Nairobi ama eneo lingine ambapo yupo ili kutusaidia kurekodi taarifa yake na kujua mashtaka atakayokabidhiwa,” alisema Ndambuki.

Mnamo Alhamisi, Juni 10, Diana Opemi Lutta kupitia ripoti aliyowasilisha katika Kituo cha Polisi cha Nyali alidai kuwa Mukhisa Kituyi alimpiga mangumi na mateke baada ya kukataa kushiriki ngono naye.

"Ripoti ya kupigwa iliyowasilishwa na Diana Opemi Lutta mnamo Mei 22, mwendo wa saa 0200. Amepigwa na mtu anayejulikana katika kijiji cha Tamarind, Mukhisa Kituyi, ambaye anadai ni mpenzi wake," ilisoma ripoti ya OB.

Ndambuki alibainisha kuwa bado Lutta anataka kuendelea na kesi hiyo dhidi ya Kituyi, akiongezea kuwa polisi wako kwenye harakati ya kuwasilisha faili hiyo kwa Idara ya Upelelezi kwa hatua zaidi kuchukuliwa.

Kipusa huyo alisema alijeruhiwa kwenye mguu wake wa kushoto na alishauriwa na polisi kutafuta matibabu uchunguzi ukiendelea kuhusu kisa hicho.

“Polisi walimshauri atafute matibabu kwa hatua zaidi baada ya kupewa fomu ya P3 ambayo ilijazwa na Hospitali ya Coast General,” ilisema ripoti ya polisi.

Mnamo Alhamisi, Juni 10, Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai alimuita Kituyi kufuatia madai hayo.

READ ENGLISH VERISON

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke