Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wamkamata afisa wa zamani wa GSU miaka 2 baada ya kuiba benki

Pingu 1024x769 Polisi wamkamata afisa wa zamani wa GSU miaka 2 baada ya kuiba benki

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: Radio Jambo

Wapelelezi kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) mnamo Jumanne, Julai 11, walimkamata afisa wa zamani wa Kitengo cha Huduma ya Jumla (GSU) anayeaminika kuwa ndiye aliyepanga wizi wa benki miaka miwili iliyopita.

DCI, katika taarifa yake, ilifichua kuwa afisa huyo wa zamani wa polisi alihusika na wizi wa mchana katika benki uliotokea Matuu mnamo Julai 2021.

Katika kisa cha hivi punde, afisa huyo wa zamani wa GSU anadaiwa kutekeleza visa 9 vya wizi wenye ghasia katika maeneo tofauti nchini.

"Afisa huyo wa zamani wa polisi alidhihirika haswa katika kisa cha wizi wa benki wakati genge lake la watu watano lilipora benki hiyo na kutoweka na bunduki mbili aina ya AK47 zilizonyang'anywa silaha na maafisa waliokuwa wakiisimamia," taarifa kutoka DCI ilisoma kwa sehemu.

Idara hiyo ilidokeza kuwa wapelelezi wake walifuatilia kesi hiyo kwa muda wa miaka miwili, kipindi ambacho pia waliondoa genge la mshukiwa.

Kabla ya kumkamata afisa huyo wa zamani wa GSU, bunduki moja iliyoibwa ilipatikana na watu kadhaa walikamatwa.

Wapelelezi hao pia walikiri kukabiliwa na changamoto za kumsaka bwana huyo kwa sababu alijificha kwenye kivuli wakati wenzake walipokamatwa au kufariki dunia wakati wa majibizano ya risasi na polisi.

Hata hivyo, hawakukata tamaa na msako huo na mnamo Jumanne, Julai 11, walipata bunduki ya pili katika eneo la Takaungu kaunti ya Kilifi.

Ilikuwa wakati wa oparesheni ya Takaungu ambapo maafisa hao walifahamu kuwa askari huyo wa zamani alikuwa amejificha huko Gilgil.

“Uchunguzi wa awali kufikia sasa umemhusisha na visa 9 vya wizi vilivyoripotiwa katika kaunti za Mombasa, Kwale, Kilifi na Machakos.

Chanzo: Radio Jambo