Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wamkamata Kasisi mlaghai - DCI

Polisi Wamkamata Kasisi Mlaghai   DCI Polisi wamkamata Kasisi mlaghai - DCI

Tue, 30 May 2023 Chanzo: Voa

Polisi wamemkamata kasisi anayeshukiwa kuilaghai kanisa ya ACK mjini Mwea, kwa madai ya ulaghai wa shilingi milioni 2 ambazo zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya kutengeneza viti vya kanisa hiyo.

Mnamo Februari 9, 2023, uongozi wa kanisa ulimpa kandarasi Mtume Blessed Gilbert Kariuki pamoja na mkewe kuleta viti 410 kanisani kabla au mwezi Aprili 10,2023, ila ‘Mtu wa Mungu’ hakuleta wala kuonekana kanisani tena.

Kama inavyoripotiwa na waumini katika kituo cha polisi cha Wang´uru mwanaume huyo aliwalaghai hela hizo kabla ya kutoweka katika upeo wa macho yao.

Kulingana na DCI, juhudu za kumsaka zimekuwa zikiambulia patupu kilichochangia kanisa kufikisha ripoti katika kituo cha polisi. Polisi aliitika wito huo na kwa bahati nzuri walifanikiwa kumkamata mshukiwa huyo.

Chanzo: Voa