Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wamfungulia mashtaka ya ugaidi Imran Khan

Imran Khan Polisi wamfungulia mashtaka ya ugaidi Imran Khan

Tue, 21 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi wa Islamabad wamemfungulia mashtaka ya ugaidi mwenyekiti wa chama cha Pakistan-Tehreek-e-Insaf (PTI), Imran Khan na viongozi wengine zaidi ya 12 kwa madai ya kuwashambulia maofisa wa polisi na kusababisha machafuko nje ya Mahakama ya Shirikisho (FJC).

Vyombo mbalimbali vya habari viliripoti vurugu kati ya wafanyakazi wa PTI na polisi Jumamosi iliyopita baada ya Khan ambaye ni waziri mkuu wa zamani wa Pakistan kufika katika mahakama hiyo kusikiliza kesi.

Inadaiwa kuwa wanachama hao walitumia mawe na vifaa mbalimbali kupambana na polisi ambapo zaidi ya maofisa 25 wa polisi walijeruhiwa.

Katika mashtaka hayo yaliyowasilishwa na ofisa wa kituo cha Polisi cha Ramna, Malik Rashid Ahmed katika idara ya kukabiliana na ugaidi ya Islamabad, anadai kuwa kiongozi huyo wa PTI na wafuasi wake walikiuka sheria ikiwa ni pamoja na kusababisha shughuli kusimamia.

Amedai wanachama wa PTI waliokuwa na silaha walipiga mawe kituo cha ukaguzi cha polisi huko Dhok, Kashmir na kuweka vizuizi vya moto barabarani.

"Umati huo ulizunguka jengo la mahakama, kuvunja milango na madirisha,” inaelezwa sehemu ya mashtaka hayo.

Katika madai hayo, wafuasi hao wanadaiwa walichoma moto magari 16 ya polisi, pikipiki nne, kuwashambulia polisi kwa fimbo sambamba na kuwaibia vifaa vyao vya kazi, bastola na Rupia 20,000.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live