Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wamchapa mgonjwa na kumjeruhi vibaya akielekea hospitalini saa za kafyu

0fgjhs5bc10ubkipp Polisi wamchapa mgonjwa na kumjeruhi vibaya akielekea hospitalini saa za kafyu

Wed, 28 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Ida Chema anaripotiwa kutendewa ukatili huo katika Kituo cha Polisi cha ParklandsKutokana na kichapo cha mbwa alichopokezwa Chema, mnamo Jumatatu, Julai 26, sasa hawezi kutembea bila msaadaMumewe Chema, Christopher Mwenda alisema mke wake alianza kukumbwa na maumivu ya kifua usiku

Polisi katika Kituo cha Polisi cha Parklands, jijini Nairobi wako motoni baada ya kumkamata, kumtandika na kumjeruhi vibaya mwanamke mmoja aliyekuwa akielekea hospitalini saa za kafyu.

Mwathiriwa, Ida Chema anaripotiwa kutendewa ukatili huo katika Kituo cha Polisi cha Parklands, gazeti la Taifa Leo limeripoti.

Kutokana na kichapo cha mbwa alichopokezwa Chema, mnamo Jumatatu, Julai 26, sasa hawezi kutembea bila msaada.

Akisimulia mahakama tukio hilo Jumanne, Julai 27, mumewe Chema, Christopher Mwenda alisema kuwa mke wake alianza kukumbwa na maumivu ya kifua usiku na kukimbizwa katika Hospitali ya MP Shah mwendo wa saa tano usiku.



Read also

David Kurgat: Yabainika Afisa Aliyefariki Dunia Baada ya Kumtembelea Mpenziwe Alikunywa Chai

Wakiwa katika safari yao hospitalini, walisimamishwa na polisi kwenye barabara ya Ojinjo.

Mwenda alimuelezea Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Kibera, Esther Boke kuwa alijaribu kuwarai polisi kumruhusu amfikishe mke wake hospitalini kisha baadaye wamkamate lakini kilio chake kilipuuzwa.

Wawili hao walikamatwa na kisha kuachiliwa siku ya Jumapili, Julai 25.

Akifika mbele ya mahakama, Chema alionekana kuwa na maumivu huku akiketi muda wote kesi hiyo ikiendelea.

Polisi ampiga risasi mgonjwa akipelekwa hospitaliniKwingineko afisa mmoja wa polisi nchini Uganda anadaiwa kumpigia risasi jamaa mmoja aliyekuwa akisafirishwa kwenye pikipiki kwenda hospitalini.

Afisa huyo anasemekana alikuwa akipiga doria mjini Kampala wakati kisa hicho kilitokea siku ya Jumapili, Julai 25, majira ya usiku.

Kwa mujibu wa taarifa za Daily Monotor, Jedi Onyango, 49, alikuwa amempigia simu daktari wake kulalama kuhusu hali yake ya kiafya na akamuagiza aende hospitalini.

Polisi huyo anasemekana kumfyatulia risasi mara mbili Onyango kwa madai kwamba alikuwa amekiuka amri ya kutotoka nje.

Read also

Freeman Mbowe: Mpinzani Mkuu Tanzania Augua Akiwa Kwenye Seli

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke