Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wahofiwa kupoteza maisha baada ya boti kuzama Ziwani

Ziwa Tanganyikarr Polisi wahofiwa kupoteza maisha baada ya boti kuzama Ziwani

Fri, 24 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watatu wakiwemo maafisa wawili wa polisi hawajulikani walipo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kupinduka katika ziwa Victoria nchini Kenya.

Wawili hao na afisa wa mamlaka ya mapato wanasemekana kuwa sehemu ya timu ya maafisa wanane waliokuwa wakiendesha operesheni ya pamoja katika ziwa hilo.

Boti yao ilipinduka mwendo wa saa sita usiku yapata mita 200 (futi 660) kutoka ufuo wa Mugabo magharibi mwa Kenya, polisi wamenukuliwa na vyombo vya habari vya ndani.

Watano waliokolewa na shughuli ya kuwatafuta maafisa waliotoweka inaendelea

Silaha tatu na risasi ambazo maafisa waliotoweka walikuwa nazo bado hazijapatikana, polisi walisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live