Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wafyatua mabomu ya kutoa machozi Kenya

Polisi Wafyatua Mabomu Ya Kutoa Machozi Kenya Polisi wafyatua mabomu ya kutoa machozi Kenya

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Polisi wa kutuliza ghasia nchini Kenya wamewarushia mabomu ya kutoa machozi wakazi wa kitongoji duni kikubwa zaidi katika mji mkuu wa Nairobi, ili kuwazuia kuandamana hadi katikati mwa jiji kwa ajili ya maandamano yaliyopangwa na upinzani.

Mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi anasema kuna msururu mkubwa wa polisi mjini humo na njia za kuelekea kwenye makazi rasmi ya rais zimezuiwa.

Baadhi ya wazazi wamechagua kuwazuia watoto wao wasiende shuleni siku ambayo masomo yalikusudiwa kuanza tena baada ya mapumziko ya katikati ya muhula.

Milolongo mifupi imeshuhudiwa katika mitaa ya Nairobi kabla ya maandamano yaliyopangwa.

Barabara zinazoelekea Ikulu zimefungwa huku polisi wakielekeza baadhi ya magari kurejea yalikotoka na kutafuta njia mbadala.

Nchini Kenya, vyombo vya habari vya ndani vinaripoti kwamba kumekuwa na msururu mkubwa wa maafisa wa usalama katika mji mkuu, Nairobi, siku ya Jumatatu hasa karibu na majengo muhimu ya serikali.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga anapanga maandamano nchi nzima dhidi ya Rais William Ruto na serikali yake.

Bw Odinga anasema kuwa maandamano hayo yatakuwa dhidi ya gharama ya juu ya maisha na kile anachokiita urais haramu.

Chanzo: Bbc