Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wachunguzwa baada ya wanahabari kufyatuliwa vitoa machozi Kenya

Polisi Wachunguzwa Baada Ya Wanahabari Kufyatuliwa Vitoa Machozi Kenya Polisi wachunguzwa baada ya wanahabari kufyatuliwa vitoa machozi Kenya

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Vyombo vya habari nchini Kenya vinasema polisi wameanzisha uchunguzi wa ndani dhidi ya afisa mmoja aliyevalia nguo za kiraia ambaye alionekana kuwarushia vitoa machozi waandishi wa habari katika eneo lisilo wazi wakati wa maandamano ya kuipinga serikali wiki iliyopita.

Video ya mtandaoni inayoonesha afisa huyo akivunja kioo cha mbele na kuwarushia waandishi wa habari mabomu ya machozi ndani ya gari ililaaniwa na wanadiplomasia na wanasiasa.

Gari hilo lilikuwa sehemu ya msafara ulioandamana na kiongozi wa upinzani Raila Odinga alipokuwa akipitia vitongoji vya Nairobi kuwakusanya wafuasi wake.

Siku ya Jumanne Inspekta Jenerali wa Polisi Japheth Koome alisema kwamba visa vyote vinavyodaiwa kuwa vya utovu wa nidhamu wa polisi wakati wa maandamano vinachunguzwa.

"Polisi akivunja kioo cha gari? Kuhusu maafisa wote, suala lolote la utovu wa nidhamu linaloletwa kwetu linachunguzwa na tunachukua hatua. Nilipokea malalamiko hayo na yanashughulikiwa," alinukuliwa na The Star news.

Chanzo: Bbc