Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi waanzisha uchunguzi kufuatia mauaji ya mlinzi Moi Avenue

0fgjhs2js79oip43ag Polisi waanzisha uchunguzi kufuatia mauaji ya mlinzi Moi Avenue

Sat, 1 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Ripoti zinaonyesha kuwa watu wanaoshukiwa kuwa majambazi walivamia bohari hilo Ijumaa, Aprili 30 alasiri

- Mmiliki mwenye bohari hiyo ambaye ana leseni ya bastola alionekana akiwafyatulia risasi majangili hao ila alikosa na risasi hiyo ikampata mlinzi huyo kichwani, na kumuua papo hapo

-Wakati wa tukio hilo, raia mwingine ambaye alikuwa akipita alipigwa risasi kimakosa na baadaye alikimbizwa hospitalini

Polisi jijini Nairobi wanachunguza kisa ambapo mtu asiyejulikana alimpiga risasi bawabu aliyekuwa akilinda bohari moja Moi Avenue.

Ripoti zinaonyesha kuwa watu wanaoshukiwa kuwa majambazi walivamia bohari hilo Ijumaa, Aprili 30 alasiri.

Mmiliki mwenye bohari hiyo ambaye ana leseni ya bastola alionekana akiwafyatulia risasi majangili hao ila alikosa na risasi hiyo ikampata mlinzi huyo kichwani, na kumuua papo hapo.

Umati wa watu ulikusanyika eneo la tukio huku kila mmoja akitaka kujua kilichokuwa kimetokea

Mwili wake baadaye ulipelekwa katika makafani ya City kusubiri upasuaji.

Wakati wa tukio hilo, raia mwingine ambaye alikuwa akipita alipigwa risasi kimakosa na baadaye alikimbizwa hospitalini.

Kulingana na afisa wa polisi ambaye hakutaka kutajwa alisema kisa hicho kinachunguzwa.

Alisema mshukiwa tayari amendakisha taarifa kwa maafisa wa polisi.

Kwingineko watu wawili wanaodaiwa kuwa majambazi walipigwa risasi na kuuawa na maafisa wa polisi waliokuwa wakishika doria katika eneo la Stage 56 la Kawangware Jumatano, Aprili 28.

Kulingana na ripoti ya polisi, washukiwa hao wawili walikuwa miongoni mwa genge la majangili watatu ambao walimshambulia na kumpora mtu asiyejulikana wakiwa wamejihami kwa bastola.

Ripoti hiyo ilisema maafisa wa polisi waliokuwa wakishika doria waliwaamuru wajisalimishe, lakini badala yake walianza kuwafyatulia risasi.

Washukiwa wawili waliuawa naye wa tatu alitoroka akitumia pikipiki iliyokuwa na nambari feki ya usajili.

Bastola moja na risasi zilipatikana na kukabidhiwa wataalam wa DCI kukagua silaha hiyo.

Miili ya wawili hao ilipelekwa katika makafani ya City.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke