Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wa Zambia wawatia mbaroni wahamiaji haramu 15 wengine

DC2F8526 22CE 49FE B180 EAEF80CC89CC.jpeg Polisi wa Zambia wawatia mbaroni wahamiaji haramu 15

Tue, 21 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi la kaskazini mwa Zambia jana Jumatatu lilitanga kuwatia mbaroni wahamiaji haramu 15 ambao takriban wote ni raia wa Ethiopia katika jitihada za kukabiliana na wimbi kubwa la wakimbizi wanaoitumia Zambia kama njia ya kuelekea maeneo mengine ikiwemo Afrika Kusini.

Vyombo vya habari vimeripoti habari hiyo na kusema kuwa 14 kati ya wahamiaji hao walioingia Zambia kinyume cha sheria ni raia wa Ethiopia na mwingine anasadikiwa ni Msomali. Wahamiaji hao wote ni wanaume wenye umri wa kati ya miaka 17 na 28 na walikutwa ndani ya lori na trela iliyosajiliwa nchni Tanzania ambayo kazi yake ni kubeba madini ya salfa.

Akitoa ufafanuzi kuhusu habari hiyo, Danny Mwale, naibu msemaji wa polisi ya kaskazini mwa Zambia amesema: "Lori hilo na trela lenye namba za usajili T636 DVR na T565 DVP kwa utaratibu, yalikamatwa kama saa nne na nusu asubuhi jana Jumapili kando ya Barabara ya Great North. Wakati askari walipokuwa wanapita kwenye lori hilo walimwona mtu akichungulia kutoka garini na kuwalazimisha askari hao kulisimamisha na kufanya upekuzi mara moja na kuwakamata wahamiaji hao 15.

Katika taarifa yake aliyoitoa katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka, Mwale amesema, polisi pia wanawashikilia dereva wa lori hilo aliyetambulika kwa jina la Muhammad Juma Lango, 37, na dereva mwenzake, Shabani Issa, 30, wote kutoka Dar-es-salaam Tanzania.

Zambia hivi karibuni imekuwa ikikabiliwa na matukio mengi ya uhamiaji haramu, ikitumiwa kama kituo muhimu cha kusafirishia wahamiaji haramu wa nchi za Pembe ya Afrika ambao wanaahidiwa "malisho ya kijani" katika ncha ya kusini mwa bara la Afrika yaani Afrika Kusini.

Serikali ya Zambia imesema imeanzisha kampeni maalumu ya kuzima wimbi la wahamiaji hao haramu na inawahesabu wanaeondesha biashara hiyo kuwa ni wafanya magendo ya binadamu ambayo ni haramu kimataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live