Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wa Uganda wapiga marufuku mikutano ya Bobi Wine

Polisi Wa Uganda Wapiga Marufuku Mikutano Ya Bobi Wine Polisi wa Uganda wapiga marufuku mikutano ya Bobi Wine

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Polisi nchini Uganda wamepiga marufuku mikutano ya kisiasa inayoandaliwa na kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi, ambaye pia anajulikana kama Bobi Wine, kutokana na ukiukaji wa utaratibu wa umma na kumchafua rais.

Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Tumusiime Katsigazi Jumatano alisema mtu mmoja amefariki na wengine 10 kujeruhiwa vibaya katika mikutano ya chama cha National Unity Platform (NUP).

Bw Katsigazi aliwaonya wafuasi wa NUP dhidi ya kile alichokitaja kuwa "mawazo ya kundi la watu...dhidi ya raia na wasimamizi wa usalama".

Polisi pia walimshutumu Bw. Kyagulanyi kwa kuchochea makundi katika mikutano yake iliyoanza Jumatatu.

Bw Kyagulanyi, hata hivyo, ameapa kuendelea na mikutano na kuwataka wafuasi wake "kusubiri ishara". Anatumia mikutano hiyo kuinua uungwaji mkono mashinani kabla ya uchaguzi mkuu wa 2026.

Chanzo: Bbc