Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wa Uganda walitibua njama ya kulipua makanisa - Museveni

Polisi Wa Uganda Walitibua Njama Ya Kulipua Makanisa   Museveni Polisi wa Uganda walitibua njama ya kulipua makanisa - Museveni

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Polisi wa Uganda walizuia shambulio la bomu dhidi ya makanisa lililofanywa na kundi la waasi la Allied Democratic Forces (ADF) katikati mwa wilaya ya Butambala, Rais Yoweri Museveni amesema.

Wanamgambo hao wanaohusishwa na Islamic State siku ya Jumapili walikuwa wakipanga kutega mabomu mawili katika makanisa ya Kibibi, karibu kilomita 50 kutoka mji mkuu Kampala, Bw Museveni aliandika kwenye mtandao wa X, ambao zamani ilijulikana kama Twitter.

Lakini vifaa hivyo "viliripotiwa kwa polisi na kuhariwa", aliongeza.

Rais alisema mabomu hayo yalifichwa kama mifumo ya anwani na zawadi kwa wachungaji wa eneo hilo. Ziliripotiwa na wananchi waliokuwa na mashaka alisema.

Mapema siku hiyo hiyo, Bw Museveni alisema vikosi vya Uganda vilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya ngome nne za ADF katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

"Inaonekana idadi kubwa ya magaidi waliuawa," rais alisema.

Alionya kwamba ADF wanaotoroka "wanaingia tena Uganda na kujaribu kufanya vitendo vya kigaidi vya kubahatisha".

Mwezi Juni, wanamgambo wa ADF waliwaua watu 42, wakiwemo wanafunzi 37 katika shule ya upili magharibi mwa Uganda karibu na mpaka na DR Congo.

Lilikuwa moja ya mashambulizi mabaya zaidi ya ADF nchini humo.

Chanzo: Bbc