Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wa Kiislamu wavamia 'harusi ya wapenzi wa jinsia moja' nchini Nigeria

Polisi Wa Kiislamu Wavamia 'harusi Ya Wapenzi Wa Jinsia Moja' Nchini Nigeria Polisi wa Kiislamu wavamia 'harusi ya wapenzi wa jinsia moja' nchini Nigeria

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: bbc

Jeshi la polisi la Kiislamu kaskazini mwa mji mkuu wa Nigeria limewakamata Waislamu 19, likiwatuhumu kuhudhuria harusi ya wapenzi wa jinsia moja.

Kikosi hicho kilivamia sherehe ya ndoa huko Kano baada ya kupewa taarifa, msemaji wake Lawal Ibrahim Fagge alisema.

Wanandoa hao ambao walikuwa bado hawajaweka viapo vyao, walifanikiwa kukimbia na polisi walikuwa wakiwatafuta, aliongeza.

Kano ina idadi kubwa ya Waislamu, ambapo mfumo wa kisheria wa Kiislamu unafanya kazi pamoja na sheria za kilimwengu.

Vitendo vya mahusiano ya jinsia moja ni haramu chini ya mifumo yote miwili ya kisheria katika Nigeria nzima, ambapo wale wanaoishi kaskazini ni Waislamu na watu wa kusini ni Wakristo.

Kikosi cha polisi cha Kiislamu cha Kano kinajulikana kama Hisbah na kinatekeleza kanuni kali za maadili.

Bw Fagge aliambia BBC kwamba jeshi la polisi halikukusudia kuwaadhibu waalikwa 15 wa kiume na wanne wa kike waliokamatwa wakati wa uvamizi huo siku ya Jumapili.

Badala yake, kundi hilo - ambalo alisema ni pamoja na watu wa jinsia moja - lilikuwa likipata "ushauri", na wazazi au walezi wao walikuwa wamehimizwa kujitokeza.

"Tutachunguza njia ya mabadiliko kabla ya kuwafungulia mashtaka mahakamani. Kwanza tunawashauri, na kuwahusisha wazazi na tuna matumaini kuwa watabadilisha mtindo wao wa maisha," msemaji wa Hisbah alisema.

Mahakama za Kiislamu za Kano hazijawahi kumhukumu mtu yeyote kwa kuwa mpenzi wa jinsia moja.

Bw Fagge alisema kuwa watu 18 waliohudhuria sherehe hizo za harusi mwaka jana wameachiliwa baada ya kutia sahihi hati iliyotoa "ahadi kwamba watabadili mtindo wao wa maisha".

Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Nigeria kwa muda mrefu yamekuwa yakifanya kampeni ya kutaka haki za wapenzi wa jinsia moja ziheshimiwe, lakini kuna upinzani mkubwa dhidi yake katika nchi ambayo Waislamu na Wakristo wengi wanashikilia maadili ya kidini.

Chanzo: bbc