Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wa Kenya waanza uteuzi wa maafisa wa kupelekwa Haiti

Polisi Wa Kenya Waanza Uteuzi Wa Maafisa Wa Kupelekwa Haiti Polisi wa Kenya waanza uteuzi wa maafisa wa kupelekwa Haiti

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Huduma ya Polisi ya Kenya imeanza uteuzi wa maafisa watakaotumwa Haiti huku wakisubiri idhini ya bunge.

Barua ambayo BBC imeiona kutoka kwa Inspekta Jenerali wa Polisi inaomba kwa dharura orodha ya majina kutoka kwa Kitengo cha maalum cha GSU.

Pia inaeleza mahitaji yanayohitajika na maafisa watarajiwa.

Miongoni mwa masharti hayo ni huduma ya chini ya miaka 5, wenye umri kati ya miaka 20-55, ufahamu wa lugha ya Kiingereza, na uwezo wa kushika silaha kwa usalama.

Katiba ya Kenya inaihitaji serikali kupata idhini kutoka kwa bunge kabla ya kupeleka vikosi nje ya nchi.

Hoja bungeni inayojadili misheni ya Haiti haikuweza kuanza wiki iliyopita kutokana na kukosekana kwa idadi ya wabunge kuijadili.

Akizungumza Jumapili, Waziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa Kithure Kindiki alisema hakutakuwa na njia za mkato au ukiukaji wa katiba katika kuwatuma polisi hao Haiti.

Kenya ilijitolea kuongoza jeshi la polisi la kimataifa katika taifa hilo la Karibea ili kukomesha ghasia za magenge zinazoongezeka. Nchi hiyo iliahidi maafisa wake 1000 kusaidia kurejesha utulivu.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilitoaidhini kwa ujumbe huo kufuatia wito wa msaada kutoka kwa serikali ya Haiti.

Chanzo: Bbc