Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi, raia mmoja wakamatwa na karatasi za kura zenye tiki

Karatasi Tiki Zakamatwsa.png Polisi, raia mmoja wakamatwa na karatasi za kura zenye tiki

Wed, 10 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi eneo la Kilgoris katika Kaunti ya Narok wanazuilia watu watatu wakiwemo maafisa wawili wa polisi kwa tuhuma za kusafirishwa karatasi za kupiga kura ambazo tayari zimetiwa alama na vifaa vingine vya uchaguzi

Kupitia kwa taarifa, Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Narok Kizito Mutoro amesema kuwa washukiwa walikamatwa mwendo wa saa kumi na mbili na nusu jioni baada ya raia kufuata gari hilo na kupiga ripoti.

“Polisi walipata ripoti kutoka kwa raia ambao walisema kuwa walikuwa wamepata karatasi zilizotiwa alama katika kituo cha mafuta. Polisi walifinika eneo hilo na kupata gari aina ya Toyota Sienta lililokuwa limebeba vifaa vya uchaguzi na kupewa ulinzi na maafisa wawili wa polisi,” Mutoro alisema.

Miongoni mwa vifaa vilivyopatikana ni sahili moja ya wapiga kura ya gereza Kiligoris, madaftari mawili ya matokeo ya uchaguzi, pakiti mbili za karatasi za kupiga kura za urais na fomu nne za 35c. “Sanduku moja la kura za urais ziliharibiwa na raia.

Afisa mkuu wa uchaguzi wa eneo bunge la Trans Mara alithibitisha kuwa vifaa vilivyopatikana vilikuwa vya IEBC,” Mutoro alisema. Zingine ni fomu tano za 36c, sita za 34b, saba za 39b, nane za 35b, tisa za 36b na fomu kumi za 38b.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live