Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi mstaafu adaiwa kumpiga risasi mkewe wa miaka 63

RISASI 2222222222 Polisi mstaafu adaiwa kumpiga risasi mkewe wa miaka 63

Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa mstaafu wa polisi Joel Kiptanui anadaiwa kumpiga risasi mkewe, Sarah Chepkemoi, katika kisa cha kusikitisha huko Kuresoi Kusini

Kiptanui, ambaye anamiliki bunduki yenye leseni, inasemekana alitumia bastola yake aina ya Ceska kumpiga mkewe risasi kichwani na mkononi

Baada ya kumpiga risasi mkewe, Kiptanui alijaribu kujidhuru, na kupata jeraha la kifua ambalo hatimaye lilisababisha kifo chake wakati alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Molo

Polisi walipata bastola ya Ceska na risasi katika eneo la tukio, na miili ya wanandoa hao ilipelekwa kwenye chumba cha kuhifadi maiti kusubiri uchunguzi wa maiti

Ofisa huyo mstaafu wa polisi anadaiwa kumpiga risasi mkewe papo hapo kabla ya kujidhuru.

Akithibitisha kisa hicho, kamanda wa polisi wa Kuresoi Kusini Jeremiah Leariwala alisema kuwa Joel Kiptanui, afisa wa polisi aliyeaga dunia alikuwa mmiliki wa bunduki aliyeidhinishwa kwa kupewa leseni.

Ripoti ya Citizen Digital ilionyesha kuwa Joel Kiptanui alimpiga mkewe, Sarah Chepkemoi, kichwani na mkononi.

"Hatujui jinsi mzozo huo ulivyoibuka. Lakini tunajua Kiptanui ni mmiliki wa bunduki aliyeidhinishwa. Alitumia bastola yake aina ya Ceska," mkuu wa polisi aliripoti.

Sarah aliripotiwa kupoteza maisha papo hapo.

Je, Kiptanui alikumbana aje na mauti yake? Kiptanui alijijeruhi kifuani na kufariki kutokana na risasi alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali moja mjini Molo.

Maofisa wa polisi walitembelea eneo la tukio, ambapo walipata bastola aina ya Ceska inayodaiwa kutumika katika kisa hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live