Polisi nchini Kenya Jumatano itaufukua mwili wa mtalii Muingereza aliyefariki miaka miwili iliyopita ili kupata taarifa kuhusu kifo chake.
Luftunisa Kwandwalla, 44, kutoka Leicester nchini Uingereza alifariki Agosti 2020 katika nyumba ya kiongozi wa dhehebu la kisiri yenye utata katika mji wa mwambao wa Kenya wa Mombasa.
Sababu ya awali ya kifo chake ilitajwa kuwa ni mshituko wa moyo, lakini familia yake inadai kuwa aliuawa na mwili wake kuzikwa haraka ili kuficha ushahidi.
Mapema mwezi huu, mahakama ya Kenya iliipatia familia yake idhini ya kufanya vipimo vya maiti ili kubaini iwapo aliuawa.
Mwili wake utafufuliwa Jumatano mchana huku watu wa familia yake wakiwepo na uchunguzi wa mwili utafanyika baadaye leo.
Bi Kwandwalla aliwasili nchini Kenya akitokea Uingereza Agosti 2019 kuwatembelea watu wa familia ya mume wake.
Alitarajia kurejea Uingereza miezi kadhaa baadaye, lakini sheria za udhibitiwa Corona ulimzuia kurudi Leicester.
Ni wakati huo ambapo familia yake inasema alijiunga na dhehebu lenye utata katika mwambao wa Kenya
Familia yake inadai kwamba aliuawa baadaye nyumbani kwa mhubiri wa Kiislamu anayeshutumiwa kuendesha dhehebu la siri.