Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi auawa kwa kupigwa risasi, mwili wake wapatikana ndani ya gari lake

D29860a0292a388d Polisi auawa kwa kupigwa risasi, mwili wake wapatikana ndani ya gari lake

Tue, 6 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mwili wa konstebo John Ogweno ambaye alikuwa akihudumu katika kituo cha polisi cha Kasarani kaunti ya Nakuru ulipatikana ndani ya gari lakeMadirisha ya gari lake yalikuwa yamevunjwa, ishara kwamba yalipasuliwa kwa kugonjwa na maweRipoti ya polisi ilionyesha kwamba marehemu alipigwa risasi kwenye upande wake wa kulia wa kichwa na alifariki dunia kwa kuvuja damu nyingiUchunguzi kufuatia kifo chake umeeenzishwaAfisa mmoja wa polisi aliyekuwa akihudumu katika kituo cha polisi cha Kasarani kaunti ya Nakuru amepatikana akiwa ameuawa ndani ya gari lake.

Mwili wa Konstebo John Ongweno ulipatikana na afisa mwenzake Joseph Ologe katika eneo la kuegesha magari alipokuwa akipiga doria.

Kulingana na ripoti ya polisi, konstebo Ologe aliyapata madirisha ya gari la mwendazake lenye nambari ya usajili KBV 735 U yakiwa yamevunjwa.

Ologe alipochungulia ndani ya gari hilo, aliona mwili wake ukiwa kwenye kiti na alikuwa akivunja damu tokea kwenye pua.

Naibu kamanda wa polisi kaunti ya Nakuru Eric Wanyonyi, afisa mkuu wa upelelezi eneo hilo na OCS wa Nakuru walifika katika eneo la tukio na kuthibitisha kisa hicho.

Kulingana na ripoti hiyo ya polisi, konstebo Olego alipigwa risasi upande wa kulia wa kichwa na alifariki dunia kutokana na kuvuja damu nyingi.

Risasi ambayo haikuwa imetumika, jiwe na chuma vilipatikana katika eneo la tukio na vitatumika kama ushahidi mahakamani.

Vile vile bunduki aina ya Ceska aliokuwa akitumia marehemu haijapatikana hadi sasa, maafisa wa upelelezi wameanzisha uchunguzi dhidi ya kisa hicho.

Hata hivyo, afisa huyo hakuwa amelalamikia usalama wake na alikuwa buheri wa afya siku moja baada ya kukumbana na kifo chake.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 073248269.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke