Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Uganda kukamata wanaonunua kuanzia "Chapati" tano

Polisi Ug Polisi nchini Uganda

Fri, 20 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi katika wilaya ya Moroto kaskazini mwa Uganda wameanza kuwakamata watu wanaonunua chapati tano au zaidi, wakishuku huenda wanawalisha wezi wa mifugo katika eneo hilo, Uganda Radio Network (URN) inaripoti.

"Tumepokea taarifa kwamba wale wanaonunua chapati nyingi wanawapelekea wapiganaji misituni," Micheal Longole, msemaji wa polisi wa Karamoja, alinukuliwa URN.

Amesema kukomesha usafirishaji wa chakula kwa wezi hao huenda kukawalazimu kutoka mafichoni na kuwasilisha silaha zao.

Mwanaharakati wa amani wa eneo hilo Mark Koryang alisema mpango huo hautafaulu "Hawa wapiganaji wanaweza kuishi bila hata kula chapati," alisema. Mkazi mwingine aliiambia URN kwamba maafisa wa usalama walihitaji kufanya kazi na watu wa eneo hilo ili kukabiliana na ukosefu wa usalama katika jimbo hilo.

Bunduki 58 zimepatikana katika eneo zima tangu zoezi la upokonyaji silaha lilipoanza mnamo Julai 17, Edrine Mawanda, msemaji wa kitengo cha jeshi anayefanya zoezi hilo, aliiambia URN.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live