Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Kenya yapiga marufuku maandamano Nairobi

Maandamano Kenya Ghsz Polisi Kenya yapiga marufuku maandamano Nairobi

Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kenya limepiga marufuku maandamano katika eneo la katikati ya mkuu wa nchi hiyo, Nairobi hadi itakapotangazwa tena kufuatia wiki kadhaa za maandamano dhidi ya serikali ambayo limesema yamevamiwa na magenge ya wahalifu.

Kabla ya marufuku hiyo, mabango kadhaa yamesambwzwa mtandaoni yakihimiza waandamanaji kukusanyika katika uwanja wa Uhuru uliopo jijini humo kabla ya kuelekea Ikulu leo.

“Tuna taarifa za kuaminika kuwa magenge ya wahalifu yamepanga kutumia maandamano yanayoendelea kutekeleza mashambulizi yao ikiwa ni pamoja na uporaji,” amesema Kaimu Mkuu wa Polisi Douglas Kanja Kirocho.

Biashara jijini Nairobi zimebaki zimefungwa kwa hofu ya kurejea kwa uporaji uliofanyika wakati wa maandamano wiki iliyopita, ambapo waandamanaji walivamia Bunge na baadhi yao kuuawa na polisi.

Waandamanaji wanamtaka Rais Ruto ajiuzulu na kufanyika mabadiliko ya kimsingi ili kupambana na rushwa na kushughulikia uongozi mbovu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live