Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Kenya wazuia maandamano ya kuunga mkono Palestina

Polisi Kenya Wazuia Polisi Kenya wazuia maandamano ya kuunga mkono Palestina

Fri, 26 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi nchini Kenya wametumia mabomu ya machozi na kuwakamata watu kadhaa wakati wa maandamano ya amani ya kuunga mkono Palestina yaliyofanyika Alhamisi jijini Nairobi.

Taarifa zinasema Polisi wa Kenya walirusha vitoa machozi kutawanya maandamano hayo ya amani ambayo yalifanyika kwa mshikamano na Wapalestina wakati huu wa vita vya mauaji ya kimbari vya utawala haramu wa Isarel dhidi ya Wapalestina wa Gaza. Maandamano hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kenyans4Palestine, yanaripotiwa kuwa yalikuwa na kibali kilichotolewa na mamlaka kwa ajili ya mkusanyiko wa amani lakini yalikabiliwa na askari polisi wakati waandamanaji walipoweka kambi nje ya Ubalozi wa Ujerumani mjini Nairobi.

Waandamanaji hao walikuwa wakilalamikia hatua ya Ujerumani kuunga mkono jinai za utawala wa Isarel dhidi ya Wapalestina. Ujerumani imetangaza kuwa iko pamoja na utawala wa Kizayuni wa Israel katika kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya utawala huo katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).

Maandamano hayo yamefanyika wakati waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani akiwa nchini Kenya katika ziara ya siku nne barani Afrika.

Polisi walituma mabomu ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji ambapo wanaharakati watatu walikamatwa.

Lali Yusuf, mmoja wa washiriki katika maandamano hayo ameliambia Shirika la Habari la Anadolu la Uturuki kwamba: "Tulikusanyika kwa amani kuonyesha uungaji mkono wetu kwa watu wa Palestina, na inakatisha tamaa kushuhudia majibu mazito kama haya kutoka kwa mamlaka. Tulikusudia kuongeza ufahamu na kuonyesha mshikamano na Wapalestina.

Hatua ya polisi Nairobi kuwakamata waandamanaji na kuzuia maandamano ya amani imelaaniwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu. Shirika la kutetea hakiza binadamu la Amnesty International limetoa taarifa likielezea wasiwasi wake kuhusu kutumiwa polisi wenye silaha na mabomu ya machozi ili kuvuruga mijumuiko halali ya raia.

Amnesty imesema: "Jeshi la Polisi lilijulishwa kwa mujibu wa sheria. Waandamanaji walikusanyika kihalali na kwa amani. Sheria za Kenya zinasistiza kuwa maoni ya wananchi yanastahili kuheshimiwa." Shirika hilo aidha limetaka wale waliokamatwa waachiliwe huru mara moja bila masharti.Taarifa zinasema waliokamatwa wameachiliwa kwa dhamana na watafunguliwa mashitaka kortini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live