Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Picha za polisi wa kike anayeshtumiwa kuua wanaume 2 na kutoroka

Cdd1cbcdfd743318 Picha za polisi wa kike anayeshtumiwa kuua wanaume 2 na kutoroka

Wed, 7 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

DCI ilionya kuwa koplo Caroline Kangongo amejihami na ni mtu hatari sana na kuomba umma kuwa wangalifuKangongo ndiye mshukiwa mkuu katika kisa cha mauaji kilichotekea Nakuru na Juja, kaunti ya Kiambu Kwa sasa yuko mbioni baada ya kuwaua wanaume wawili na bado nia yake kutenda kitendo hicho haijabainika

Katika kudurusu picha zake, hakuna mtu anaweza kuamini kuwa Caroline Kangongo ana uwezo wa kumuua yeyote kinyama.

Hata hivyo, afisa huyo wa polisi yuko mafichoni baada ya kuhusishwa na mauaji ya kinyama ya wanaume wawili Nakuru na mwingine Juja.

Taarifa kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI) ilisema kuwa Kangongo amejihami na ni mtu hatari sana na kuomba umma kuwa wangalifu hususan wanaume.

Hii hapa baadhi ya picha za Kangongo

1. Kangongo anashukiwa kumpiga risasi na kumuua konstebo Joseph Ogweno ambaye alipatikana ameuawa ndani ya gari lake Jumatatu, Julai 5.

Mwili wa Ogweno ulipatikana na afisa mwenzake sajini Joseph Ologe ambaye alikuwa anatembea karibu na eneo hilo la kuegesha magari.



2. Siku moja baada ya kutenda kitendo hicho cha kinyama, DCI inasema alimuwekea mtego mwanamume mwingine katika hoteli moja iliyoko Juja ambapo pia alimpiga risasi na kumuua.

Anadaiwa kumuua mwanamume wa pili Jumatatu, Julai 5, siku moja baada ya kumuangamiza Ogweno.

3. Maafisa wa polisi wanamsaka na bado yuko mbioni akiwa amejihami na hivyo ni hatari.DCI imewaonya wanaume kuwa wangalifu zaidi kwani anawavizia kuingia hotelini kisha anawaua kinyama.



4. DCI inaomba umma kutoa habari zozote kuhusu mshukiwa huyo na pia kuwa makini kwa sababu amejihami.

Idara hiyo inayoongozwa na George Kinoti ilionya umma dhidi ya kumuamini ama kumupa makao.

Kama TUKO.co.ke ilivyoripotia awali, konstebo Ogweno alipigwa risasi kwenye upande wa kushoto wa kichwa chake.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke