Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Picha za Rais Uhuru kabla ya kuomoka na kuwa bazuu

5d04a8b8dc62ca9f Picha za Rais Uhuru kabla ya kuomoka na kuwa bazuu

Sun, 25 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Ilikuwa ni uchaguzi wa 2007 ambapo Uhuru alipata kichapo na ikamuuma sana na kufanya apotee uwanja wa siasaMoses Kuria alikuwa mmoja wa wale ambao walipanga jinsi Uhuru atapoteza uchaguzi huoKwa sasa Rais amekomaa kisiasa na kuonekana kuelewa kadi za kisiasa kama alivyokuwa profesa wa siasa MoiPicha za Rais Uhuru Kenyatta kabla ya kuwa bazuu zimeibuka mtandaoni na kuwakumbusha wengi kuwa safari ni maisha.

Katika picha hizo, Uhuru anaonekana akiwa mnyonge wakati ambapo alikuwa akisaka kura za kuwa mbunge wa Gatundu Kusini.

Ni picha ambazo zimewavunja wengi mbavu wakiamini kuwa kwa kweli 'watu hutoka mbali' kabla ya kuafikia wanachomiliki leo.

Kijana wa Mama Ngina anaonekana akiwa amevalia kabuti na kofi huku akichapa kampeni amejawa na imani wakazi watamfanya mheshimiwa wao.

Kwenye kampeni hizo, kundi la vijana wanaandamana na Uhuru ingawa ni ngumu kujua mgombea ni nani kwani wote wamechapa.

Read also

Ubinafsi wa baadhi ya wanasiasa unahatarisha kwenye mapambano dhidi ya COVID-19

Upekuzi wa meza ya TUKO.co.ke umeonyesha kuwa picha hizo ni za uchaguzi wa 1997 ilipokuwa mara ya kwanza kwa Uhuru kuingiza mguu katika siasa kama mgombea.

Ni uchaguzi ambao ulimwacha na machungu rohoni baada ya kupokezwa kichapo na mpinzani wake licha ya kuwa familia ya Kenyatta ilikuwa imefungulia mfereji wa minofu kwa wakaazi.

Mbunge wa sasa wa Gatundu Kusini Moses Kuria, alikuwa mmoja wale ambao walitoa mbinu za kuhakikisha kuwa Uhuru anabwagwa kwenye uchaguzi huo.

Kuria alikuwa kwenye kambi ya mpinzani wa Uhuru aliyejulikana kama Moses Muhia na walipogundua kuwa familia ya Kenyatta ilikuwa na mifuko mizito kushawishi wapiga kura kumchagua kijana wao, Kuria alicheza kama yeye.

Waliibuka na mbinu ambapo Muhia alitekwa nyara na gari lake kutupwa mtoni na kisha wakaanza porojo kulaumu famlia ya Kenyatta.



Read also

Kitu Ilikuwa Safi: Tume ya IEBC Yasema Kuhusu Uchaguzi wa Kiambaa



Wakazi walijawa na ghadhabu za ni kwa nini familia hiyo iamue kumtesa kijana maskini kama Muhia na ndipo waamua kuipa funzo.

Siku ya kura walijaza kikapu za Muhia kabla yake kujitokeza jioni na kudai ameachiliwa huru na waliokuwa wamemteka nyara.

Hivyo ndivyo Uhuru alipoteza kiti hicho na ikamuuma sana kiwango cha kuahidi kuachana na siasa kabisa.

Hata hivyo, muda mchache baadaye aliyekuwa rais Daniel Moi alimsaka na kumuingiza bungeni 2001 kupitia uteuzi.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke