Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Picha za Peter Njiru aliyeuawa kwa kupigwa risasi na konstebo Caroline Kangogo

289e70ac6b168c47 Picha za Peter Njiru aliyeuawa kwa kupigwa risasi na konstebo Caroline Kangogo

Thu, 8 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Caroline Kangogo ameolewa na afisa mwenzake na kwa pamoja wamejaliwa watoto wawiliKulingana na upelelezi kutoka Idara ya DCI, Kagongo anadaiwa kumuua Peter Njiru kwa kumpiga risasi wakiwa kwenye hoteli moja mtaani Juja Julai 5 Mwili wa Njiru ulipatikana na wahudumu wa hoteli hiyo siku iliyofuata Wazazi wa Kangogo wamemusihi ajisalimishe kwa polisi mahali popote alipoMaafisa kutoka idara ya Upelelezi, DCI wanaendelea kuchunguza kisa ambapo afisa wa polisi Konstebo Caroline Kangogo anashtumiwa kuwauwa wanaume wawili kwa kuwapiga risasi.

Imeripotiwa kwamba Konstebo John Ongweno na Peter Njiru walikuwa wapenzi wake wa zamani na haijabainika haswa kilichompelekea afisa huyo kukatiza maisha yao.

Kwa mujibu wa taarifa za DCI, Kangogo alikodisha chumba cha kulala akiwa na Njiru katika hoteli moja mtaani Kimbo eneo la Juja mwendo wa saa kumi jioni Julai 5.

Kangago ambaye ni mama wa watoto 2 aliondoka baadaye kwenye chumba hicho mwendo wa saa sita usiku akidai kwenda kununua dawa ya meno, tayari alikuwa ashamuua Njiru.

Mwili wa Njiru ulipatikana na mhudumu wa hoteli hiyo siku iliyofuata ukiwa na majeraha ya risasi.

Kulingana na maafisa wa upelelezi, huenda Kangogo analipiza kisasi kwa wapenzi wake wote kwa kuwaangamiza, hata hivyo bado anasakwa.

Njiru alikuwa na mke na TUKO.co.ke imeweza kukusanya baadhi ya picha zake;

Aidha, wazazi wake wamemtaka Kangogo ambaye kwa sasa yuko mafichoni ajisalimishe kwa polisi ili naye atowe taarifa yake.

Wakiwa kwenye mahojiano na runinga ya KTN, Jumatano Julai 7, babake Barnaba Kipkoech Korir aliomboleza vifo vya wawili hao na kuhakikishia famila hizo kwamba haki itatendeka.

"Tunaomba msamaha kwa familia mbili zilizowapoteza wapendwa wao kutokana na mauaji yanayodaiwa kutekelezwa na binti wetu. Tungependa kumrai mahali alipo ajitokeze na ajisalimishe kwa polisi. Yeye mwenyewe ni polisi na anaelewa sheria, tungependa sana ajisalimishe." Babake Kangogo alisema.

Kulingana na Kori, imebakia ndoto kwake yeye kuamini kwamba bintiye angetekeleza kitendo hicho cha unyama.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke