Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Picha za CCTV zaonesha mume wa mwanariadha Agnes alikuwa eneo la mauaji

Ae42549e4bba4e81 Ibrahim Rotich ni mshukiwa mkuu wa mauaji ya Agnes Tirop

Tue, 9 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mwanariadha Agnes Tirop alikutwa amefariki dunia Jumatano, Oktoba 13, ndani ya chumba chake cha kulala huko Iten.

Ripoti ya madaktari ilionesha kuwa marehemu Tirop alipigwa na kitu kizito kichwani, pamoja na kudungwa kisu mara kadhaa shingoni.

DCIO wa kaunti ndogo ya Keiyo Kaskazini Andolo Munga amesema kanda za CCTV zilionesha kuwa Tirop aliuawa alasiri ya Jumanne, Oktoba 12, 2021 Kanda za picha za CCTV zimeonesha kuwa mume wa marehemu mwanariadha Agnes Tirop, Ibrahim Rotich ni mshukiwa mkuu wa mauaji ya nyota huyo.

Picha hizo zilionyesha kuwa mshukiwa alikuwa katika eneo la uhalifu nyumbani kwake Iten siku ambayo Tirop aliuawa kikatili.

"Picha za CCTV zinajieleza wazi baada ya uchambuzi wa kitaalamu. Ina ushahidi wote wa tukio na kitendo halisi. Tunaamini hapa tuna kesi na sasa tutaendelea na mashtaka,” amesema mpelelezi huyo.

Katika ripoti ya Daily Nation, Munga alisema kuwa picha hizo zilionyesha kwa usahihi kile kilichotokea na jinsi kilifanyika hadi pale Tirop alipofariki dunia.

Hapo awali, iliripotiwa kuwa Rotich alikuwa amezuiliwa kwa siku 20 ili kuruhusu polisi kukamilisha uchunguzi kuhusu madai yake ya kuhusika katika mauaji ya mwanariadha huyo.

Rotich alifikishwa mbele ya Hakimu Charles Kutwa, ambapo upande wa mashtaka ulitaka muda zaidi wa kumzuilia.

Mahakama iliamuru mshtakiwa azuiliwe katika Kituo cha Polisi cha Railways mjini Eldoret.

Pia atafanyiwa uchunguzi wa akili katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Eldoret.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke