Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Picha ya Rais Uhuru akiwa amekasirika yazua gumzo

3f09041aee21e638 Picha ya Rais Uhuru akiwa amekasirika yazua gumzo

Fri, 24 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Picha za hafla hiyo zinamnakili Kenyatta akiwa na sura kama ya mfalme asiyetaka mchezo kwenye uongozi wakeRais anaonekana akiwa ameshika upanga wake kwenye mkono wa kushoto huku akionekana kuuma ndimu kweli kweliBaadhi ya Wakenya walihoji ni vipi Rais alionekana mtu asiye na furaha wakati wa hafla hiyoRais Uhuru Kenyatta Alhamisi September 23 aliwakumbusha wanaomchezea kuwa yeye ndiye mwenye upanga wa uongozi.

Katika hafla ya wanajeshi wa maji huko Manda Bay Rais Uhuru alionekana akiwa amejihami kwa upanga wa uongozi.

Picha za hafla hiyo zinamnakili Kenyatta akiwa na sura kama ya mfalme asiyetaka mchezo kwenye uongozi wake.

Tofauti na hafla zingine ambapo Rais huonekana akitabasamu, Alhamisi alikuwa amekaaa ngumu kweli kweli.



Wakati wa hafla hiyo ambapo Kenya Navy ilipata uhuru wa kuendeleza shughuli zake, Rais alitaka Wakenya kushirikiana na vikosi vya usalama.

Alisema changamoto za kiusalama nchini zinahitaji wananchi washirikiane na vikosi vyote ili kuhakikisha usalama unadumishwa.

"Jamii zetu na kila mwananchi ni lazima afanye wajibu wake. Na ninataka kuwaomba wote katika eneo hili wakiwemo viongozi kushirikaina na vikosi vya usalama ili kuafikia hili," alisema Rais.

Baadhi ya Wakenya kwenye mitandao walishangaa ni kwa nini Rais alionekana kukasirika kwenye mojawapo wa picha alizopigwa.

Huku akiwa ameshika upanga kwa mkono wake wa kushoto, macho yake yanaonekana kuangazia suala sugu.

Ni wazi kutokana na uso wake kuwa hana furaha au ameamua kuwa 'kiongozi kamili wa Afrika' ambao huwa hawaonyeshi tabasamu vivi hivi.

Baadhi ya viongozi haswa katika mrengo wa kisiasa wa Naibu wake wamekuwa wakikosoa uongozi wake wakisema ni wa udikteta.

Walisema aliendesha chama cha Jubilee kwa njia ya udikteta na hivyo kuwatimua wote waliokuwa wakikosoa mabaya ndani ya chama hicho.

Kwa sasa wamekuwa wakimwambia 'maliza uende' kama njia ya kuaga uongozi wake ulioanza 2013.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke