Naibu Rais wa Kenya William Ruto Almemtaka Rais Uhuru kutumia fedha zilizokuwa zimetengwa kwaajili ya kesi ya BBI zitumike kukabiliana na maambukizi ya Covid-19 nchini humo.
Ruto amesema uamuzi wa mahakama unafaa uwe kikomo cha viongozi ambao huwa na mpango wa kugawana mamlaka badala ya kushughulikia maslahi ya wananchi.
Naibu Rais William Ruto amesema uamuzi wa mahakama kuhusu rufaa ya BBI ni ushindi kwa Wakenya na katiba.
Akihutubia vyombo vya habari Jumamosi Agosti 21, Ruto aliwapa heko majaji wa Mahakama ya Rufaa akisema walionyesha ukakamavu.
Amesema mahakama ilitetea wananchi na ujumbe wao ni kuwa viongozi wanafaa kushughulikia Wakenya.
"Hakuna aliyeshinda au kushindwa. Washindi ni Wakenya na katiba. Nawapa heko majaji kwa ukakamavu wao kuilinda katiba, Mungu awabariki," alisema DP Ruto.
"Ni wakati sasa haswa kwa viongozi wa kisiasa waweke tofauti kando na kuungana katika kuwafanyia kazi wananchi wa kawaida. Hili linafaa kufanywa kma vile siasa za BBI zilifanywa," alisema Ruto
DP alisema serikali inafaa kushughulikia suala la maradhi ya Covid-19 haraka ili kufufua uchumi.
"Hili litawezekana tukitumia mali ambayo ilikuwa imetengewa shughuli za Covid-19," alisema Ruto kwenye taarifa yake.
Ruto amesema amefanya vikao na wabunge wake na kuamua kuwa watazingatia miswada ya kuwasaidia wananchi bungeni.
Ruto alisema ni wakati pia serikali izingatie njia za kuhakikisha kuwa mamilioni ya vijana nchini wanapata kazi.
Alikashifu viongozi ambao alisema wanaongozwa na azma ya kujinufaisha na vyeo badala ya kuwasaidia mamilioni ya Wakenya.
"Ni lazima tuanza kufikiria kuhusu maslahi ya Wakenya badala ya kuongea kuhusu kugawana mamlaka miongoni mwa viongozi wachache," alisema Ruto.