Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paul Kagame na Rais Samia kujadili mahusiano ya Kibiashara

Samia Rwanda Rais Samia akiwasili nchini Rwanda

Mon, 2 Aug 2021 Chanzo: BBC

Rais wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan anafanya ziara ya siku mbili nchini Rwanda ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu kuingia madarakani mwezi wa tatu mwaka huu.

Ziara hiyo imeelezwa kuwa ya kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Hakuna maelezo yaliyotolewa na serikali ya Rwanda kuhusu ziara hiyo lakini kulingana na vyombo vya habari vya upande wa serikali, Rais Samia anatarajiwa kuzuru jumba la kumbukumbu ya mauaji ya kimbari la Gesozi mjini Kigali kabla ya kukutana kwa mazungumzo na mwenyeji wake Rais Paul Kagame.

Pande mbili zinatarajia kutia saini hati za makubaliano na kuzungumza na vyombo vya Habari.

Chanzo: BBC