Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Papa ataka suluhu Niger

Papa Francis Alazwa Hospitalini Akiwa Na Maambukizo Ya Kupumua Papa ataka suluhu Niger

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ameelezea matumaini yake ya kupatikana kwa suluhu ya amani katika mgogoro wa Niger kufuatia mapinduzi ya Rais yaliyofanyika katika Taifa hilo la Afrika Magharibi.

Imeripoti kuwa Papa amewaambia Waumini katika uwanja wa St Peters kwamba anafuatilia matukio hayo kwa wasiwasi akiunga mkono ombi la kuwa na amani nchini humo na udhabiti katika Kanda nzima ya Sahel.

Ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kupata suluhusu ya amani haraka iwezekanavyo katika mzozo huo kwa manufaa ya Wananchi wa Niger.

Mwezi uliopita, Kiongozi wa utawala wa kijeshi Abdourahamane Tchiani, alimpindua Rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohamed Bazoum, hadi sasa Bazoum, Mkewe na Mtoto wake wa kiume wamewekwa katika kifungo cha nyumbani katika Mji mkuu wa Niger uitwao Niamey.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live