Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Papa Francis atoa wito wa kusitishwa vita nchini Sudan

Hivi Sio Vita, Huu Ni Ugaidi, Anasema Papa Kuhusu Mzozo Wa Israel Na Hamas Papa Francis atoa wito wa kusitishwa vita nchini Sudan

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

aa.

Papa Francis, ameziomba pande hasimu kukomesha mapigano, aliyosema yamesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu na maafa kwa raia wasio na hatia.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa, ni imani yake kuwa viongozi wanaopigana watasikia mwito wake na kurejea katika meza ya mazungumzo ili kupata suluhu ya kudumu.

Aidha Kiongozi wa Kaniisa Katoliki Duniani amezungumzia mizozo inayoendelea nchini Msumbiji, Ukraine, Israel na Palestina, akiwataka viongozi wa dunia kuwajibika kikamilifu katika kutafuta suluhu ya yanayoendelea.

Mwito wake wa kukomeshwa viita nchini Sudan unakuja wakati huu, juhudi za kidiplomasia zikiwa zimeshindwa kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo kati ya jeshi la Serikali na wapiganaji wa RSF. Majenerali mahasimu nchinii Sudan

Mapigano ya silaha yalianza huko Sudan Aprili 15 mwaka jana kati ya jeshi la nchi hiyo linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al Burhan na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) chini ya uongozi wa Kamanda Hamdan Dagalo ambapo hadi sasa juhudi za upatanishi za kimataifa za kuhitimisha mapigano hayo na kuzishawishi pande hasimu kuketi kwenye meza ya mazungumzo zimegonga mwamba.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) linasema kuwa, vita vya majenerali wa kijeshi vya kuwania madaraka nchini Sudan vimewalazimisha mamia kwa maelfu ya watu kukimbilia nchi jirani.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mashirika ya misaada ikiwemo jumuiya ya misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini yanatafuta ufadhili wa haraka wa kuwasafirisha watu wanaokimbia mapigano nchini Sudan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live